Kundi la Usafiri wa Anga la Shenyang Xinguang la China limetumia muda wa zaidi ya miaka kumi kuendeleza mfano wa pomboo wa Mto Changjiang wasio na mapezi na miale, na kuzalisha nyangumi papa wa kwanza duniani wanaofanania uhalisia. Bidhaa hizi zinaweza kuwa na aina mbalimbali za vihisi vya ubora wa maji kwa ajili ya ufuatiliaji wa ubora wa maji, kufanya uchunguzi wa hali ya ardhi chini ya maji na kwa madhumuni mengine maalum.