Lugha Nyingine
Simulizi Fupi kuhusu Rais Xi Jinping na Afrika
“China na Afrika ni marafiki wa wakati wa shida, na marafiki wa wakati wa shida hawawezi kusahauliwa. Xi Jinping ana hisia za kweli kwa watu wa Afrika. Baada ya kuapishwa kuwa Rais wa China, Rais Xi Jinping kwa mara nyingi amekutana na viongozi wa nchi za Afrika ndani na nje ya nchi, alitembelea Bara la Afrika na kuwasiliana na Waafrika na kuacha simulizi nyingi za kugusa moyo.
1.Kusalimia kwa lugha ya Kiswahili “habari”, kukumbuka msaada wa nchi za Afrika kwa maeneo ya China yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi na kusema “ni kitendo chenye ukarimu”
Mwezi Machi, Mwaka 2013, Xi Jinping alitembelea Afrika kwa ziara ya kwanza ya nje ya nchi tangu awe Rais wa China, na Tanzania ilikuwa ni kituo cha kwanza. Tarehe 25, wakati Rais Xi Jinping alipofika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius K. Nyerere, Rais wa Tanzania wa wakati huo Jakaya Mrisho Kikwete alimpokea mbele ya jengo hilo.
Rais Xi Jinping alipotembea katikati ya jukwaa la Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius K.Nyerere, makofi ya ukarimu yalipigwa kila mahali. Katika hali motomoto ya makaribisho ya kirafiki, Rais Xi Jinping alitoa hotuba muhimu. Alisalimia kila mtu kwa salamu ya lugha ya Kiswahili “Habari” , mara watu walikuwa wanaona wako karibu naye.
Katika hotuba yake, Rais Xi Jinping alikumbuka, “baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililotokea Wenchuan, nchi za Afrika zilitoa msaada, hata nchi moja isiyo tajiri, ambayo idadi ya watu wake haifikii watu milioni 2, lakini ilitoa michango ya Euro milioni 2 kwa maeneo yaliyoathiriwa na tetemeko la ardhi, kama kila mtu wa nchi hiyo alichangia Euro moja , urafiki huo uliwafanya watu wa China kuhisi ukarimu sana.”
Wakati akihitimisha hotuba yake, hakusahau kusema maneno ya lugha ya Kiswahili “asanteni sana” kwa wasikilizaji wake.
2.Kutembelea Makaburi ya Wataalam wa China kutoa rambirambi: Urafiki kati ya China na Tanzania Udumu Milele Kizazi hadi Kizazi
Machi 25, Mwaka 2013, katika ziara yake nchini Tanzania, Rais Xi Jinping alikwenda kutembelea makaburi ya wataalam wa China kutoa rambirambi bila ya kujali manyunyu ya mvua ya siku hiyo.
Kwenye makaburi hayo yaliyopangiliwa vizuri, wataalam, mafundi na wafanyakazi wa China wapatao zaidi ya 60 ambao walijitolea mihanga katika ujenzi wa Reli ya TAZARA walizikwa hapa.
Rais Xi Jinping aliweka shada la maua meupe mbele ya makaburi na kuandika maneno kwenye daftari ya ukumbusho: “Moyo wa watu waliojitolea mihanga utaenziwa na kuwatia watu moyo daima, na urafiki kati ya China na Tanzania utadumu milele kizazi hadi kizazi.” Alisema : “majina yao ni kama reli ya TAZARA. Yatakumbukwa milele mioyoni mwa watu wa nchi za China, Tanzania na Zambia”.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma