Lugha Nyingine
Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika lafanyika nchini Benin
Wanamitindo wakiwasilisha ubunifu kwenye Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika huko Cotonou, Benin, Oktoba 28, 2023 (Picha na Seraphin Zounyekpe/Xinhua)
LOME- Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika (Fesmma), lenye lengo la kutangaza mitindo ya mavazi ya Afrika na kuonesha vipaji vya ubunifu vya wabunifu wa bara hilo, limefanyika Alhamisi hadi Jumamosi mjini Cotonou, Benin.
John Medard, mwandaaji na mkuzaji wa tamasha hilo amesema tamasha hilo la Fesmma likiwa na kaulimbiu isemayo "Mitindo ya mavazi kati ya usasa na jadi katika kuhudumia maendeleo," linalenga kutoa jukwaa la kukuza wabunifu wa Afrika, kutoa fursa ya kujieleza kupitia kazi zao na kuonyesha ubunifu wao.
Kwa mujibu wa mkuzaji huyo wa kiutamaduni, tamasha hilo siyo tu kwa wabunifu wa mitindo ya mavazi na wanamitindo pekee bali pia linatambua mchango wa watu wengine muhimu katika tasnia ya mitindo, wakiwemo warembaji, wasusi wa nywele, wapiga picha za mitindo, waongozaji wa programu za mitindo na wazalishaji wa magazeti ya mitindo.
Amesema, kwa tamasha hili la Mwaka 2023, wanamitindo, wabunifu wa mavazi na wabunifu wa mitindo wapatao 20 kutoka nchi zipatazo 15 za Afrika wameshiriki katika shughuli mbalimbali, ikiwa ni pamoja na shindano la Mwanamitindo Bora, shindano la Kijana Mbunifu wa AfrikaYoung na maonyesho ya kimataifa ya mavazi ambayo hutumika kama shughuli kuu ya tamasha hilo.
Wanamitindo wakiwasilisha ubunifu kwenye Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika huko Cotonou, Benin, Oktoba 28, 2023 (Picha na Seraphin Zounyekpe/Xinhua)
Mwanamitindo akiwasilisha ubunifu kwenye Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika huko Cotonou, Benin, Oktoba 28, 2023 (Picha na Seraphin Zounyekpe/Xinhua)
Mwanamitindo akiwasilisha ubunifu kwenye Tamasha la 15 la Mitindo ya Mavazi na Uanamitindo la Afrika huko Cotonou, Benin, Oktoba 28, 2023 (Picha na Seraphin Zounyekpe/Xinhua)
Mandhari ya Hifadhi ya Taifa ya Mazingira Asilia ya Milima ya Altun katika Mkoa wa Xinjiang, China
Kutalii Hifadhi ya Taifa ya Nairobi nchini Kenya kupitia lenzi ya kamera
Habari Picha: Watu wakitembelea Mlima Huashan katika Mkoa Shaanxi, Kaskazini Magharibi mwa China
Mandhari ya Ziwa Kanas katika Eneo la Altay, Mkoa wa Xinjiang, China wakati wa majira ya mpukutiko
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma