Lugha Nyingine
Balozi: China imejikita katika kuendeleza uhusiano wa pande mbili na Ethiopia
Kundi la wasanii la Henan lilkifanya maonyesho ya ajabu ya michezo ya sanaa ya Wushu ya China kwenye karamu iliyoandaliwa na Ubalozi wa China huko Addis Ababa, Ethiopia siku ya Jumamosi. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
ADDIS ABABA Balozi wa China nchini Ethiopia Zhao Zhiyuan alisema kuwa, China itaendelea kujikita katika kuhimiza maendeleo ya uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kiwango cha juu chini ya Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na Ethiopia.
Zhao alisema hayo kwenye karamu iliyoandaliwa na Ubalozi wa China huko Addis Ababa, Ethiopia siku ya Jumamosi, ambayo ni sehemu moja ya shughuli za kusherehekea Mwaka Mpya wa Jadi wa China.
"Tutaendelea kushirikiana na Ethiopia kusukuma ushirikiano wa kiwango cha juu wa BRI kwa kiwango kipya," Zhao amesema wakati akikaribisha wageni na kutambulisha kundi la wasanii kutoka Mkoa wa Henan, katikati mwa China.
Huku akieleza kuwa China na Ethiopia zimepandisha hadhi ya uhusiano wa pande mbili kuwa uhusiano wa kiwenzi wa kimkakati wa siku zote, na Ethiopia hivi karibuni imejiunga na BRICS, balozi huyo amesema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika biashara, uwekezaji, miundombinu, kilimo, mawasiliano, mambo ya fedha, utamaduni, elimu na nyanja zingine utaendelea kushika kasi.
"Tumeshirikiana kutekeleza Pendekezo la Maendeleo ya Dunia, Pendekezo la Usalama wa Dunia, na Pendekezo la Ustaarabu wa Dunia, na kuimarisha ushirikiano wenye matokeo halisi katika ujenzi wa pamoja wa BRI na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika," Zhao amesema.
Zhao ameongeza kuwa, China inaendelea kujikita katika kubeba majukumu yake kama nchi kubwa yenye nguvu na daima inafuata maendeleo ya amani na ushirikiano wenye manufaa kwa pande zote na nchi mbalimbali duniani.
Kundi la wasanii la Henan lilifanya maonyesho ya ajabu ya michezo ya sanaa ya Wushu ya China, opera, na sarakasi na kufurahisha wahudhuriaji, wakiwemo Wachina wanaoishi nchini humo na maofisa wa serikali ya Ethiopia.
Mwaka Mpya wa Jadi wa China Mwaka 2024, utaangukia Februari 10, na kuashiria kuanza kwa Mwaka wa Dragoni.
Kundi la wasanii la Henan likifanya maonyesho ya opera kwenye karamu iliyoandaliwa na Ubalozi wa China huko Addis Ababa, Ethiopia siku ya Jumamosi. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma