Lugha Nyingine
Hafla ya ufunguzi wa Darasa la Confucius katika Chuo Kikuu cha SUZA yafanyika Zanzibar
Hafla ya ufunguzi wa Darasa la Confucius katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) imefanyika Jumatatu katika visiwa vya Zanzibar, nchini Tanzania ambapo darasa hilo litatoa fursa nzuri kwa Wazanzibari kujifunza lugha na utamaduni wa Kichina.
Akizindua dara hilo katika ukumbi wa SUZA, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali wa Zanzibar, Lela Mohamed Mussa amesema elimu ya lugha ya Kichina itakuwa na mchango mkubwa katika kukuza mawasiliano ya kirafiki kati ya watu wa China na Tanzania.
Naye Makamu Mkuu wa SUZA Mohamed Makame Haji amesema Darasa la Confucius lililopo SUZA limeanza kutatua kero ya muda mrefu ya mawasiliano na lugha ambayo imekuwa ikikwamisha maendeleo ya kiuchumi ya Wazanzibari wanaofanya kazi au kufanya biashara nchini China kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Kaimu Balozi Mdogo wa China visiwani Zanzibar Zhang Ming amesema kuanzishwa kwa dara hilo siyo tu ni kielelezo cha urafiki kati ya serikali na watu wa China na Tanzania bali pia litatoa fursa adhimu kwa wenyeji kuelewa lugha na utamaduni wa Kichina.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma