Lugha Nyingine
Video: Balozi Ali Mchumo aeleza alivyoshuhudia mabadiliko makubwa ya China na kupongeza uhusiano wa miaka 60 wa China-Tanzania
Balozi Ali Mchumo hivi karibuni alihojiwa na waandishi wa habari wa People’s Daily Online, akieleza mabadiliko makubwa ya China aliyoyashuhudia katika miaka hii yote tangu alipoanza kufuatilia kwa karibu hali ya China na kufanya kazi Beijing, ambapo amepongeza uhusiano wa miaka 60 kati ya China na Tanzania na kutumai utaimarika zaidi katika siku za baadaye.
Balozi Ali Mchumo, ambaye alikuwa Ofisa Mwandamizi wa zamani wa Serikali ya Tanzania, alipohojiwa alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Mianzi na Mihenzirani (INBAR) lenye makao makuu yake mjini Beijing. Hivi sasa amemaliza majukumu yake ya kuwa mkurugenzi mkuu na amerudi Tanzania huku akieleza kuwa ataendelea kuwakumbuka wenzake hapa China.
“Uhusiano wa miaka 60 iliyopita ulikuwa wa hali ya kipekee kabisa... umekuwa mzuri, kuanzia waasisi wa nchi zetu hizi mbili. Kwahiyo mimi nina hakika kabisa uhusiano wetu kati ya nchi za Tanzania na China, kama ulivyokuwa katika miaka 60 iliyopita, utazidi kuimarika, na ninatumai kwamba nchi zote zitanufaika” amesema Mchumo.
Habari husika: Mkurugenzi Ali Mchumo aeleza alivyoshuhudia mageuzi makubwa ya China, atoa wito kwa nchi zinazoendelea kuiga mfano
Ali Mchumo akihojiwa na People's Daily Online. (Picha na Song Ge/People's Daily Online)
Shughuli ya kuadhimisha Siku ya Mashua ya Qintong 2024 yafanyika Jiangsu, China
Watu watoa heshima kwa marehemu kabla ya siku ya Qingming katika Mji wa Beijing, China
Msanii wa Ethiopia abuni sanaa kutokana na ufunuo wa kitabu maarufu cha China “Yi Jing”
Treni yaendeshwa katikati ya maua karibu na sehemu ya Juyongguan ya Ukuta Mkuu wa Beijing
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma