Lugha Nyingine
Kutembelea Bustani ya Akiolojia ya Magofu ya Liangzhu ya China
Bustani ya Akiolojia ya Magofu ya Liangzhu ya China inachukua eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 14.33 hivi. Makumbusho ya Ustaarabu wa Liangzhu, Bustani ya Urithi wa Mji wa Kale wa Liangzhu, Bustani ya Urithi ya Yaoshan na Bustani ya Urithi ya Laohuling kwa pamoja huunda mfumo kamili wa kuonesha thamani ya urithi wa dunia wa mji wa kale wa Liangzhu. Watembeleaji wanaweza kutazama uzuri wa ustaarabu wa Liangzhu wa miaka 5,000 iliyopita kwa kupitia uoneshaji wa mabaki ya kale, uoneshaji wa magofu katika eneo husika na shughuli nyingine za kuchangamana kwa kina na mazingira ya eneo hilo.
Bustani ya Akiolojia ya Magofu ya Liangzhu katika mwezi wa Aprili huwa inakuwa na mandhari nzuri sana, ikiwa ni kivutio cha watalii kutembelea na kufurahia uzuri wa majira ya mchipuko.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma