Lugha Nyingine
Intaneti ya kasi ya satelaiti ya obiti ya chini ya China yatumika nje?ya nchi kwa mara ya kwanza
Roketi ya Long March-2C iliyobeba satelaiti ya majaribio ya teknolojia za intaneti ya satelaiti ikirushwa kutoka Kituo cha Urushaji Satelaiti cha Jiuquan, Kaskazini-Magharibi mwa China, Desemba 30, 2023. (Picha na Wang Jiangbo/Xinhua)
BEIJING - Kampuni ya kibinafsi ya anga ya juu ya China, kwa ushirikiano na chuo kikuu cha Thailand, imefanya jaribio la kwanza la mtandao wa mawasiliano ya intaneti ya kasi ya satelaiti ya obiti ya chini kwa mafanikio nchini Thailand.
Mafanikio hayo yanaashiria matumizi na utafiti wa kwanza wa intaneti ya kasi ya satelaiti ya obiti ya chini wa China katika nje ya nchi.
GalaxySpace, ambayo ni kampuni ya kibinafsi inayotengeneza satelaiti ya mjini Beijing, ilianzisha kituo cha majaribio ya ardhini kuhusu intaneti ya kasi ya obiti ya chini katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Mahanakorn nchini Thailand. Inaweza kuchunguza kila wakati uwezo wa mawasiliano wa ishara za satelaiti ya mawimbi ya milimita katika hali ya hewa ya eneo husika.
“Ushirikiano huu unatoa jukwaa ambalo kampuni na vyuo vikuu vya nchini humo vinaweza kulitumia kutafiti mifumo ya mawasiliano ya satelaiti ya obiti ya chini, na kusaidia kuongeza maendeleo ya uwezo husika wa teknolojia wa Thailand na hali ya matumizi, amesema Liu Chang, makamu mkuu wa GalaxySpace.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma