Lugha Nyingine
BYD yatoa Toleo la 5 la gari?linalotumia teknolojia ya nishati mchanganyiko ya DM
Watu wakitembelea banda la Kampuni ya magari ya BYD kwenye maonyesho ya magari huko Xi'an, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 1, 2024. (Xinhua/Zhang Bowen)
SHENZHEN – Kampuni kubwa ya China ya kuzalisha magari yanayotumia nishati mpya (NEV) ya BYD imetoa toleo la 5 teknolojia ya nishati mchanganyiko ya DM (dual mode) kwa magari ya kutumia nishati mchanganyiko za mafuta na betri ya kuchajiwa ambayo yanaweza kuendesha kwa umbali wa kilomita 2,100 baada ya kuchajiwa.
Kwa teknolojia hiyo, magari hayo ya nishati mchanganyiko ya BYD yanaweza kuongoza duniani kote katika mfululizo wa viashirio muhimu, kufikia ufanisi wa joto wa asilimia 46.06, matumizi ya mafuta ya lita 2.9 kwa kila kilomita 100 hata ikiwa katika hali ya upungufu wa umeme, na umbali wa kuendeshwa wa kilomita 2,100, mwenyekiti wa BYD Wang Chuanfu amesema kwenye hafla ya uzinduzi huko Xi'an, mji mkuu wa Mkoa wa Shaanxi, kaskazini magharibi mwa China, siku ya Jumanne usiku.
Umbali huo umefikiwa chini ya hali ya magari yenye betri iliyojaa na tangi la gari lililojaa kikamilifu mafuta ya petroli.
Kwenye hafla hiyo, BYD pia ilizindua aina mbili za magari yanayotumia teknolojia mpya, Qin L DM-i na Seal 06 DM-i, ambayo zinatumia theluthi moja tu ya mafuta yanayotumiwa na magari ya jadi na umbali wa kuendesha zaidi ya mara tatu. Bei za magari hayo ni kati ya yuan 99,800 (kama dola 14,000 za Marekani.) hadi yuan 139,800.
Wang amesema kuwa BYD ina imani katika kuongoza maendeleo ya kimataifa ya teknolojia ya magari yanayotumia nishati mseto na kuendeleza mageuzi ya kijani ya tasnia ya magari duniani.
Kampuni hiyo ya kutengeneza magari yenye makao yake makuu mjini Shenzhen, China imeuza jumla ya magari zaidi ya milioni 3.6 ya kutumia nishati mseto.
Katika miezi minne ya kwanza ya Mwaka 2024, uzalishaji na mauzo ya China ya magari yanayotumia nishati mpya yaliongezeka hadi kufikia magari milioni 2.985 na milioni 2.94, mtawalia, kwa mujibu wa Shirikisho la Viwanda vya Magari la China.
Takwimu hizo zinawakilisha ukuaji wa mwaka hadi mwaka wa asilimia 30.3 na asilimia 32.3, shirikisho hilo limesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma