Lugha Nyingine
Kuwekeza Xinjiang, China: Samaki wa Mlima Tianshan “waogelea” ?Duniani
Eneo la ufugaji wa samaki wa samoni la Xinjiang Tianyun. (Picha na Li Xinyang/People’s Daily Online)
Katika muongo uliopita, samaki wa samoni wa tani nyingi “wameogelea” kutoka Wilaya ya Nilka ya Eneo linalojiendesha la Kabila la Wakazakh la Ili, Mkoa wa Xinjiang wa China kwenda katika nchi nzima ya China na sehemu mbalimbali duniani.
Meneja mkuu wa kampuni ya kilimo cha oganiki ya Xinjiang Tianyun, Li Chunyu amejulisha kuwa, ili kuhakikisha ubora, kampuni hiyo imechukua hatua ya kupungua idadi ya samaki wanaozaliana na kukuzwa kwenye eneo maalumu.
Kupunguza uwezo wa uzalishaji kunatokana na kujiamini. Mkoa wa Xinjiang una rasilimali bora za maji baridi, ambayo ni safi, yaliyopoa na yenye oksijeni nyingi.
“Sababu ya wauzaji samaki wa ndani na nje ya China wanasifu bidhaa zetu, ni kwamba samaki wa samoni tunaozalisha na kukuza, jamii ya “triploid rainbow trout”, wana mahitaji ya juu sana kwa mazingira ya ukuaji.” Li ameeleza, akiongeza kuwa ubora wa samaki wanaokuzwa katika mazingira kama hayo ni wa uhakika.
Ubora wa hali ya juu wa samaki unategemea siyo tu mazingira bora ya kipekee ya asili, bali pia uvumbuzi wa teknolojia.
Kampuni hiyo imevumbua mfumo wa kuzaliana na kukua kwa samaki wa mizingo ya wavu ambayo ni rafiki kwa mazingira, na kuongoza kazi ya kuunda viwango vya kwanza nchini China vya mizingo hiyo ambayo ni rafiki kwa mazingira; na pia imevumbua na kutumia roboti ya kwanza nchini China ya kusafisha uchafuzi majini......
Mnamo mwaka 2023, Xinjiang ilizalisha samaki bora wa samoni wa tani 6,700, ikichukua moja ya tatu ya uzalishaji wa jumla wa samaki wa samoni wa maeneo yasiyo kando ya bahari bara ya China.
Samaki wa samoni ni mfano wa juhudi za Xinjiang za kuhimiza maendeleo ya hali ya juu ya uvuvi. Kwa sasa, uendelezaji na utumiaji wa rasilimali za uvuvi katika maeneo ya maji ya asili ya Xinjiang unaongezeka kwa nguvu kubwa zaidi mwaka hadi mwaka, na uendelezaji uvuvi wake kwenye maeneo ya maji baridi unaonyesha mwenendo wa kukua kwa kasi. Mwaka jana, uzalishaji wa bidhaa za majini wa Xinjiang ulikuwa tani 183,900, ukichukua nafasi ya kwanza kati ya mikoa mitano ya Kaskazini Magharibi mwa China.
“Tunajiandaa kushiriki kwenye Maonyesho ya nane ya China-Eurasia, na kwa kupitia maonesho mbalimbali ya China na ya kimataifa, tuwafanye samaki wa Tianshan ‘waogelee’ mbali zaidi” amesema Li.
Mizingo ya wavu ambayo ni rafiki kwa mazingira ya ikolojia. (Picha na Li Xinyang/People’s Daily Online)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma