超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Mradi wa Kijiji cha Teknolojia za Kisasa wa Huawei wazinduliwa Kusini mwa Zambia

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2024

Picha hii iliyopigwa Julai 5, 2024 ikionesha paneli za nishati ya jua kwenye kituo kidogo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua, kikiwa ni sehemu ya mradi wa Kijiji cha Teknolojia za Kisasa unaofadhiliwa na kampuni ya Teknolojia ya Huawei ya China huko Namwala, Zambia. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)

NAMWALA – Zambia imezindua mradi wa kijiji cha teknolojia za kisasa siku ya Ijumaa katika wilaya ya Kusini ya Namwala, ambao umefadhiliwa na kampuni ya Teknlojia ya Huawei ya China.

Mradi huo unaojumuisha mnara wa mawasiliano na mfumo wa kuzalisha umeme kwa nishati ya jua unaoweza kutoa nishati kwa nyumba nyingi, ni mradi wa kwanza wa aina yake nchini Zambia.

“Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa Kampuni ya Teknolojia ya Huawei Tawi la Zambia kwa uungaji wake mkono, ambayo inaendana na ajenda ya kidijitali ya serikali yetu ili kuleta maendeleo kwa maeneo ya vijijini,” amesema Rais Hakainde Hichilema wa Zambia kwenye hafla ya uzinduzi.

Katika hafla hiyo, kampuni hiyo ya teknolojia ya China imetia saini mkataba wa makubaliano na serikali ya Zambia ili kuanzisha vijiji 100 vya teknolojia za kisasa katika majimbo 10 ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Wang Sheng, kaimu balozi wa China nchini Zambia, uanzishaji huo wa vijiji 100 vya teknolojia za kisasa unatazamiwa kutoa umeme na ufikiaji wa huduma ya intaneti kwa wanavijiji 400,000 na kuzalisha nafasi mpya za ajira zaidi ya 5,000.

Wanafunzi wakionekana wakati wa uzinduzi wa mradi wa kijiji cha teknolojia za kisasa unaofadhiliwa na kampuni ya teknolojia ya Huawei ya China huko Namwala, Zambia, Julai 5, 2024. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)

Picha iliyopigwa Julai 5, 2024 ikionesha paneli za nishati ya jua kwenye kituo kidogo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua kikiwa ni sehemu ya mradi wa kijiji cha teknolojia za kisasa unaofadhiliwa na kampuni ya teknolojia ya Huawei ya China huko Namwala, Zambia. (Picha na Martin Mbangweta/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha