Lugha Nyingine
Baraza la uhifadhi wa kidijitali wa mali ya urithi wa kitamaduni lafunguliwa Beijing
Wageni wakihudhuria mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni mjini Beijing, China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Fang Sixian)
Mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni (CHCD) chini ya mada ya "Weka Sura Mpya: Uvumbuzi wa Teknolojia Wahimiza Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi", limeanza Jumanne mjini Beijing, ambapo mikutano miwili itafanyika sambamba ambayo itafuatilia zaidi teknolojia mpya na aina mbalimbali za uhifadhi wa kidijitali wa mali ya urithi, huku mijadala ya wanajopo na shughuli mbalimbali zikiwa zimepangwa.
Wajumbe zaidi ya 300 kutoka nchi na maeneo 20 wanahudhuria mkutano wa baraza hilo litakalofanyika kwa siku nne, ambapo ripoti na mada zaidi ya 100 za kitaalamu zinazohusu nyanja mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa.
Akihutubia mkutano wa ufunguzi, Yang Bin, naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Qinghua cha China, amesema kwamba anaamini mijadala ya mwanzo iliyofanyika katika mkutano wa baraza hilo itakuwa na matokeo ya kuhimiza uhasama katika maendeleo ya mali ya urithi wa kitamaduni, sayansi na teknolojia, elimu na maeneo mengine, na kuleta thamani kubwa kwa jamii.
Xie Bing, naibu mkuu wa Idara ya Mabaki ya Kale ya Kitamaduni ya China, amesema maendeleo ya haraka ya teknolojia ya kidijitali yanaleta fursa zisizo na kifani za uhifadhi wa mali ya urithi wa kitamaduni. Amekaribisha nchi nyingi zaidi kujiunga na Shirikisho la Mali ya Urithi wa Kitamaduni la Asia ili kufanya mawasiliano na ushirikiano zaidi.
Hafla ya utiaji saini pia imefanyika kwenye hafla ya ufunguzi wa Maabara ya Pamoja ya China na Ugiriki juu ya Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi, na mashirika kadhaa kutoka China na Ugiriki yameshiriki kwenye hafla hiyo.
Mkutano wa kwanza wa Baraza la CHCD ulifanyika Mwaka 2010.?
Wageni wanaohudhuria mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni wakitazama mabango mjini Beijing, China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Fang Sixian)
Wageni wakihudhuria mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni mjini Beijing, China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Fang Sixian)
Mgeni anayehudhuria mkutano wa saba wa Baraza la Kimataifa la Uhifadhi wa Kidijitali wa Mali ya Urithi wa Kitamaduni akizungumza kwenye mahojiano na waandishi wa habari mjini Beijing, China, Julai 16, 2024. (Xinhua/Fang Sixian)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma