Lugha Nyingine
Ndege ya China ya kupaa?na kutua nchi kavu na majini?AG600?yakamilisha majaribio chini ya mazingira yenye halijoto ya juu na unyevunyevu mwingi
Ndege ya zima moto ya AG600M ikichota maji kwenye majaribio ya kuchota na kudondosha maji mjini Jingmen, Mkoa wa Hubei, katikati ya China, Septemba 27, 2022. (Xinhua/Wu Zhizun)
BEIJING - Ndege kubwa ya kupaa na kutua nchi kavu na majini ya AG600 iliyoundwa kwa kujitegemea na China imekamilisha majaribio ya kuweza kuhimili hali joto ya juu na unyevu mwingi, Shirika la Viwanda ya Anga la China (AVIC) limesema siku ya Alhamisi.
AG600 imefanyiwa majaribio hayo, ambayo yalidumu saa karibu 2.5, siku ya Jumanne katika uwanja wa ndege wa Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, Mashariki mwa China. Mifumo yake yote ilifanya kazi vyema wakati wa kipindi cha majaribio, imesema AVIC.
Kabla ya majaribio hayo ya safari, ndege hiyo iliwekwa wazi juani kwa saa tano katika mazingira yenye joto la wastani wa nyuzi joto zaidi ya 35 na unyevu wa asilimia zaidi ya 44.
Halijoto ya juu na unyevunyevu mwingi hupima mfumo wa majimaji wa ndege, na ni sehemu kuu ya mchakato wa uidhinishaji wa AG600.
Kwa mujibu wa AVIC, ndege ya AG600 inalenga kupata cheti cha idhini ya aina yake mwishoni mwa mwaka huu.
Mwezi Februari mwaka huu, AG600 ilikamilisha majaribio ya safari ya wakati wa hali ya hewa ya baridi katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China.
Kisha ndege hiyo ilifanya majaribio ya safari ya usiku kwa mfululizo, na majaribio mengine mengi ya safari za ndege hiyo kama vile urekebishaji wa kasi ya ndege wakati wa safari na kasi ya kawaida ya ndege kuweza kupaa, imesema AVIC.
Baada ya majaribio hayo ya sasa ya safari ya ndege katika halijoto ya juu na unyevu mwingi huko Nanchang, ndege hiyo itasafiri hadi kituo cha majaribio ya ndege za kiraia huko Pucheng, Mkoa wa Shaanxi, kaskazini-magharibi mwa China, kampuni hiyo imeongeza.
Familia hiyo ya ndege kubwa ya kupaa na kutua nchi kavu na majini ya AG600 inaundwa kuwa sehemu ya vifaa muhimu vya kisasa vya safari ya anga ili kuimarisha uwezo wa uokoaji wa dharura nchini China, Shirika la AVIC ambalo ni muundaji wa ndege hiyo limesema.
Ndege kubwa ya kupaa na kutua nchi kavu na majini ya AG600 ya China ikikamilisha safari yake ya kwanza ya majaribio ya kuruka usiku kwenye kituo cha majaribio ya ndege za kiraia huko Pucheng, Mkoa wa Shaanxi, Kaskazini-Magharibi mwa China, Mei 7, 2024. (Shirika la Mambo ya Anga la China/ Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma