Lugha Nyingine
Jukwaa la huduma zote katika sehemu moja la China lafungua ofisi nchini Tanzania
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri akizungumza kwenye Tafrija ya Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji kati ya Tanzania na China jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 20, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)
DAR ES SALAAM –Mfumokazi wa Huduma ya Kisheria kwa Saa Moja wa Shirika la sheria la Yingke Global la China, ambao ni jukwaa la huduma zote katika sehemu moja la China umefungua rasmi ofisi yake nchini Tanzania ili kuwapa wateja huduma mwafaka na uungaji mkono sahihi kati ya maeneo mbalimbali, lugha mbalimbali, tamaduni mbalimbali na taaluma mbalimbali.
Ufunguzi huo uliofanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania imeenda sambamba na Tafrija ya Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji kati ya Tanzania na China, ambayo ililenga kuzidisha uhusiano wa kiuchumi, kuhimiza maendeleo endelevu, na kutoa fursa za kunufaishana.
Kwenye hafla hiyo iliyohudhuriwa na ujumbe wa watu kutoka serikalini na sekta binafsi za China na Tanzania zikiwemo kampuni zaidi ya 20 kutoka Tanzania na kampuni 13 kutoka China, kulishuhudiwa kutiwa saini kwa mkataba wa makubaliano kati ya Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Gilead Teri na Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kimataifa ya Shirika la Sheria la Yingke, Mei Xiangrong.
Mei amesema Mfumokazi wa Huduma ya Sheria kwa Saa Moja wa Shirika la Sheria la Yingke Global huwapa wateja kote duniani huduma za kitaalamu kuanzia za sheria, uhasibu, kodi, ushauri, uwekezaji na mambo ya fedha, uunganishaji wa kampuni na mitaji na kununua kutoka sekta za kilimo, madini, utalii wa utamaduni, na sayansi na teknolojia.
"Ninafuraha kufanya kazi nchini Tanzania kwa sababu Afrika ni siku za baadaye, na China na Afrika zinaweza kufanya kazi pamoja ili kufikia ukuaji wa uchumi imara," amesema Mei.
Teri amesema Tafrija hiyo ya Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji kati ya Tanzania na China imetoa fursa kwa viongozi wa serikali, viongozi wa wafanyabiashara na wataalamu wa sekta hiyo kufanya mazungumzo kuhusu mageuzi ya sera na mifumo ya udhibiti ambayo inaweza kuboresha mazingira ya biashara na kuvutia wawekezaji wengi kutoka nje hasa kutoka China.?
Mkuu wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kimataifa wa Shirika la Sheria la Yingke, Mei Xiangrong, akizungumza kwenye Tafrija ya Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji kati ya Tanzania na China jijini Dar es Salaam, Tanzania, Julai 20, 2024. (Xinhua/Emmanuel Herman)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma