Lugha Nyingine
China yatangaza hatua mpya za kutumia vifaa vipya badala ya vifaa vya zamani
Picha hii iliyopigwa tarehe 24 Aprili 2024 ikionyesha mstari wa kuunganisha sehemu za magari yanayotumia nishati mpya (NEV) wa BYD, kampuni inayoongoza nchini China ya kuunda NEV, kwenye kiwanda cha BYD mjini Zhengzhou, Mkoa wa Henan, Katikati ya China. (Xinhua/Li Jianan)
BEIJING – Kamati ya Kitaifa ya Maendeleo na Mageuzi ya China (NDRC), ambayo ni mpangaji mkuu wa uchumi wa China imetangaza siku ya Alhamisi hatua mpya za mpango wa kutumia vifaa vya aina mpya badala ya vifaa vya zamani, ambapo yuan takriban bilioni 300 (dola za Kimarekani karibu bilioni 42) ambazo ni dhamana maalum za kitaifa za muda mrefu zitatengwa ili kuhimiza kubadilisha upya vifaa na vyombo kwa kiasi kikubwa na kutumia vifaa na vyombo vya aina mpya badala ya vile vya zamani.
Mpango huo wa kutumia vifaa na vyombo vya aina mpya badala ya vile vya zamani, utapanuliwa kwa vifaa vya nishati ya umeme, lifti za zamani, meli zinazofanya kazi, malori, mashine za kilimo na mabasi yanayotumia nishati mpya, NDRC imesema.
Bajeti ya serikali kuu ya China pia itatoa ruzuku ya riba yenye thamani ya yuan bilioni 20 moja kwa moja kwa taasisi za fedha katika kuunga mkono kubadilisha upya zana na vifaa na kuboresha kiteknolojia zana na vifaa hivyo, NDC imeeleza.
China tayari imekamilisha ujenzi wa mfumo wa sera kwa ajili ya kuhimiza kubadilisha upya vifaa na zana kwa kiasi kikubwa, na kutumia vyombo vya aina mpya badala ya vile vya zamani, wakati serikali za mitaa 31 ya mikoa au maeneo yanayojiendesha zote zimetoa mpango wa utekelezaji.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma