Lugha Nyingine
Makamu mwenyekiti wa chama tawala cha Tanzania ajiuzulu
Chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Bw. Abdulrahman Kinana ameandika barua ya kuomba kujiuzulu.
Taarifa iliyotolewa na chama hicho imesema mwenyekiti wa CCM, Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Tanzania ameridhia ombi lake hilo la kujiuzulu.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia amesema alipenda Bw. Kinana aendelee na wadhifa huo, lakini ametoa ombi lake la kujiuzulu tangu muda mrefu uliopita akitaka kupata nafasi ya kupumzika.
Rais Samia ameongeza kuwa chama hicho kitaendelea kukuza uzoefu ulioonyeshwa na Bw. Kinana wakati alipokuwa madarakani.
Bw. Abdulrahman Kinana aliteuliwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM mwezi Aprili mwaka 2022 akichukua nafasi ya Bw. Philip Mangula.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma