Lugha Nyingine
Shirika la ndege la Ethiopia kuimarisha miundombinu na uwezo kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za China
(CRI Online) Julai 31, 2024
Shirika la Ndege la Ethiopia linafanya kazi ili kuimarisha miundombinu na uwezo wake kupitia mradi wa kujenga makao makuu yake mapya kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za China.
Mradi huo ulioko katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa, umepangwa kukamilika mwezi Agosti mwaka 2026, na unatarajiwa kuimarisha hadhi na uwezo wa shirika hilo katika nyanja ya usafiri wa anga.
Mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo sita makuu katika hatua ya kwanza, yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 67.8.
Meneja Mtendaji wa mradi huo kutoka kampuni ya ujenzi na uhandisi ya China (CCECC), Bw. Wang Peng amesema ujenzi wa mradi huo ulianza mwezi Desemba mwaka jana, na kwamba hadi sasa umetoa nafasi 500 za ajira kwa wenyeji.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma