Lugha Nyingine
Waziri wa Ulinzi wa China asema PLA liko tayari kuzuia na kuteketeza shughuli zozote za ufarakanishaji
Tafrija kubwa ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 97 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) ikifanywa na Wizara ya Ulinzi ya China kwenye Jumba la Mikutano ya Umma la Beijing la China, Julai 31, 2024. (Picha na Yang Jiahui /Xinhua)
BEIJING - Waziri wa Ulinzi wa China Dong Jun siku ya Jumatano kwenye tafrija kubwa ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 97 tangu kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China (PLA) iliyoandaliwa na Wizara ya Ulinzi ya China mjini Beijing, amesema kwamba Jeshi la Ukombozi wa Umma la China liko tayari kuzuia na kuteketeza shughuli zozote za ufarakanishaji na kulinda ipasavyo maslahi ya taifa la China.
Dong amesema hivi sasa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China liko kwenye kipindi kipya muhimu cha kihistoria katika kuimarisha ujenzi wa jeshi na kwamba maofisa na askari wake wote wanaahidi kutii kabisa na kufuatilia zaidi hali ya kuwa tayari kupigana vita, na siku zote kujikita katika kutimiza lengo la miaka 100 ya Jeshi la Ukombozi wa Umma la China itakapofika Mwaka 2027. Amesema, Jeshi la Ukombozi wa Umma la China linapenda kujiunga pamoja na majeshi ya nchi mbalimbali katika kufanya ushirikiano wa kirafiki wenye matokeo halisi, kuanzisha mfumo wa usalama ulio wa haki na usawa ambao watu wote wanaweza kunufaika nao, na kujenga Dunia yenye amani ya kudumu na usalama popote.
Leo Tarehe Mosi Agosti ni Siku ya maadhimisho ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ukombozi wa Umma la China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma