Lugha Nyingine
Xi awatia moyo wanaviwanda wa Hong Kong kutoa mchango mkubwa katika ujenzi?wa mambo ya kisasa wa China
BEIJING - Rais wa China Xi Jinping kwenye barua ya majibu kwa wajumbe wa wanaviwanda wengi wa Hong Kong ambao ni wazaliwa wa Ningbo wa Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China wakiwemo pamoja na Pao Yue-kong na Run Run Shaw, wanaojulikana sana ng’ambo, amewatia moyo wanaviwanda hao wa Hong Kong wajiunge zaidi katika mageuzi na maendeleo ya taifa, na kutumia nguvu yao bora kwa kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Wajumbe hao, wakiwemo Pao Pui-hing na Chao Kee-Young, ambao ni wa kizazi cha wajasiriamali watangulizi wa Hong Kong waliozaliwa Ningbo, hivi karibuni walimwandikia barua Rais Xi kuripoti juu ya juhudi zao za kuunga mkono maendeleo ya taifa na kuelezea dhamira yao ya kusukuma ujenzi wa mambo ya kisasa wa nchi yao mama.
Kwenye barua hiyo ya majibu, Rais Xi amesifu sana uzalendo wao na mchango waliotoa kwa ajili ya maendeleo ya maskani yao ya awali na nchi yao kupitia juhudi za kuanzisha shughuli na kufanya uvumbuzi na kutoa michango kwa mambo ya elimu.
“Jitihada za kujenga nchi kubwa na kutimiza ustawishaji wa taifa katika mambo yote kupitia ujenzi wa mambo ya kisasa wa China zinahitaji juhudi za pamoja za watu wote wa China,” Rais Xi amesema, akitoa wito kwao kutoa mchango mpya kwa ajili ya kutimiza Ndoto ya China ya ustawishaji wa taifa.
Viongozi wa China wamekuwa wakiweka umuhimu zaidi kwa wanaviwanda wa ng'ambo waliozaliwa Ningbo. Mwaka 1984, Rais wa wakati huo Deng Xiaoping alitoa maagizo ya kujitahidi kupata uungaji mkono wao kwa maendeleo ya Ningbo. Wakati alipofanya kazi Zhejiang, Xi alionyesha mara kwa mara kujali na kuwa na matarajio kwa wanaviwanda wa ng'ambo waliozaliwa Ningbo.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma