Lugha Nyingine
Tanzania yapongeza mradi wa msaada wa China kwa kudhibiti ugonjwa wa kichocho
DAR ES SALAAM, - Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nchini Tanzania imepongeza mradi wa China wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho, ikisema umesaidia kutokomeza ugonjwa huo katika visiwa hivyo vya Bahari ya Hindi.
Kwenye ziara ya kutembelea Mradi wa Msaada wa China wa Kudhibiti Ugonjwa wa Kichocho Zanzibar, viongozi mbalimbali akiwemo Habiba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya ya Zanzibar na Mratibu wa Wizara ya Afya Kisiwani Pemba, Khamis Bilali Ali wameelezea pongezi na shukrani zao za dhati.
Wataalamu wa China wanaosimamia mradi huo waliwasilisha mazingira na maendeleo ya mradi huo wa awamu ya pili na muundo wake wa kufanya kazi.
Habiba ameishukuru Serikali ya China kwa kuunga mkono kwa dhati kazi ya afya ya Zanzibar kwa miaka mingi na kushukuru kikundi cha wataalamu wa kudhibiti ugonjwa wa kichocho kutoka China kwa juhudi zao za kutokomeza ugonjwa huo kisiwani Zanzibar na kuwasaidia watu wa sehemu hiyo kuondokana na madhara yatokanayo na ugonjwa huo.
Habiba ameeleza matumaini yake kuwa Taasisi ya magonjwa ya vimelea ya Jiangsu, kitengo mahususi cha kutekeleza mradi huo, itaongeza uhamishaji wa teknolojia, kutoa msaada zaidi katika kuwaandaa wafanyakazi wa Zanzibar, kukuza vipaji bora vya kudhibiti ugonjwa wa kichocho, na kufikia lengo la kutokomeza kichocho haraka iwezekanavyo.
Pia, amesema faida zinazowezekana za mikakati jumuishi ya udhibiti wa kichocho, kama vile kutokomeza konokono kupitia uingiliaji kati wa kiikolojia na usambazaji wa maji salama, zitasaidia watu wa eneo hilo kuboresha mazingira yao ya maisha na kupunguza uwezekano wa kupata maji yaliyoambukizwa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma