Lugha Nyingine
Treni za kutumia umeme za SGR za Tanzania zaanza kutoa huduma kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma
(CRI Online) Agosti 02, 2024
Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania amezindua rasmi huduma za treni ya kutumia umeme ya Reli ya Kiwango cha Kimataifa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma jana Alhamisi.
Safari za majaribio kati ya miji hiyo miwili zilianza mwezi uliopita.
Rais Samia amepanda treni hiyo na kuwasili Dodoma baada ya safari ya saa tatu na nusu. Amesema, mwendokasi mkubwa wa treni hiyo utapunguza kwa kiasi kikubwa muda wa kusafiri na kurahisisha usafiri wenye ufanisi wa watu na mizigo nchini Tanzania.
Rais Samia amesema Serikali imeagiza mabehewa 1,430 ya mizigo, ambayo yataimarisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam hadi maeneo ya ndani na nchi jirani zisizo na bandari, ikiwemo Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma