Lugha Nyingine
Rais wa Zambia atoa wito wa kufanyika makubaliano ya kimataifa kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema ametoa wito wa kuwepo kwa maelewano ya haraka ya kimataifa ili kumaliza mgogoro kati ya Russia na Ukraine.
Amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Ivanovych Kuleba ambaye anatembelea nchini Zambia.
Amesema kuwa mgogoro wa Russia na Ukraine unahitaji kutatuliwa kwa njia za amani, akisisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa ili kuongeza hali ya utulivu na amani katika eneo hilo.
Aidha ametoa wito wa kuimarishwa kwa uhusiano wa pande mbili kati ya Zambia na Ukraine, hasa katika maeneo ya biashara na uwekezaji, kwa manufaa ya watu wa nchi hizo mbili.
Kwa upande wake, waziri wa mambo ya nje wa Ukraine ameishukuru Zambia kwa mshikamano wake wa kisiasa na nchi yake, na kumpongeza Hichilema kwa kushiriki katika juhudi za kidiplomasia kumaliza mgogoro huo.
Ameongeza kuwa lengo la ziara yake barani Afrika ni kuendelea kujenga uhusiano na nchi za Afrika, akisisitiza haja ya kutafuta fursa mpya kati ya Zambia na Ukraine kwa kuimarisha ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pande zote mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma