Lugha Nyingine
Mjumbe wa China asisitiza wito wa kusimamishwa mara moja kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza
UMOJA WA MATAIFA - Dai Bing, Kaimu Balozi wa Ujumbe wa Kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa, siku ya Jumatano katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kudumisha ahadi za WPS (amani na usalama kwa wanawake) katika muktadha wa kuharakisha upunguzaji wa operesheni za amani amesisitiza wito wa kusimamisha mapigano mara moja katika Ukanda wa Gaza.
"Tunapozungumza sasa, mgogoro katika Ukanda wa Gaza umekuwa ukiendelea kwa zaidi ya siku 300, huku watu zaidi ya 10,000 wameuawa na wanawake na wasichana wa Palestina zaidi ya milioni moja wanakabiliwa na njaa," Balozi Dai amesema.
Balozi huyo amesisitiza wito kwa pande zote kuitikia "makubaliano ya wengi ya jumuiya ya kimataifa" na kuhimiza kwa pamoja utekelezaji "kikamilifu na wenye ufanisi" wa maazimio husika ya Baraza la Usalama kwa ajili ya kufikia usimamishaji wa mapigano wa mara moja katika Ukanda wa Gaza, ili kukomesha balaa ya ubinadamu, na kuzuia mgogoro usienee zaidi.
Katika hotuba yake, balozi huyo amesisitiza kuwa juhudi zote za kuzuia na kutatua migogoro na kuweka mazingira ya amani kwa raia, wakiwemo wanawake, ni sharti la kwanza la kuhimiza utekelezaji wa ajenda ya WPS.
"Bila kujali operesheni za amani zitapitia mipito au marekebisho gani, kuhimiza utatuzi wa kisiasa wa matatizo ya mitafaruku kunapaswa kuwa jukumu la msingi kila mara," amesema.
China inaunga mkono Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusikiliza vya kutosha na kuheshimu matakwa ya nchi husika, na kwenye msingi huo, kuandaa mipango ya mpito na mikakati ya kuondoka iliyobainishwa na kuweza kutekelezwa kihalisi, tena kutilia maanani kufuata mikakati ya maendeleo ya nchi husika na sekta zao zenye kipaumbele, ili kuhakikisha mipango ya mpito inatekelezwa kwa hatua madhubuti, amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma