超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Barabara iliyojengwa na China yabadilisha maisha ya akina mama katika maeneo ya vijijini katikati mwa Kenya

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 08, 2024

Picha ya droni iliyopigwa tarehe 3 Aprili 2024, ikionyesha mandhari ya jiji la Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

Picha ya droni iliyopigwa tarehe 3 Aprili 2024, ikionyesha mandhari ya jiji la Nairobi, Kenya. (Xinhua/Han Xu)

NAIROBI – Simulizi ya Mercy Nyaguthii inaakisi hali ya akina mama wengi wa nyumbani, ambao walibaki nyumbani, wakisubiri waume zao wawape mahitaji.

Mzaliwa wa kijiji chenye utulivu katikati mwa Kenya, Kaunti ya Nyeri, Nyaguthii, ambaye ni mama wa watoto watatu, angekuwa akifanya kazi duni kwa mapato kidogo au mbaya zaidi, akitumia muda mwingi wa siku bure, kwa kukosa kazi.

Miaka mitatu iliyopita, hata hivyo, alijiunga na idadi inayoongezeka ya wanawake walioanzisha biashara ndogondogo kando ya barabara ya Kenol-Sagana-Marua baada ya mradi wa kuboresha barabara hiyo kuwa ya njia nane za kupitisha magari kwa njia nne kila upande, uliotekelezwa na Kampuni ya Uhandisi wa Usafirishaji ya Jiangxi China, Oktoba Mwaka 2020.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta (wa pili kulia), akiwa na Waziri wa Uchukuzi James Macharia (wa tatu kushoto) na maafisa wengine, wakikagua sehemu ya barabara ya Kenol-Sagana-Marua katika Kaunti ya Nyeri, Kenya, Aprili 26, 2021. (Picha na Charles Onyango/Xinhua)

Rais wa Kenya wa wakati huo Uhuru Kenyatta (wa pili kulia), akiwa na Waziri wa Uchukuzi James Macharia (wa tatu kushoto) na maafisa wengine, wakikagua sehemu ya barabara ya Kenol-Sagana-Marua katika Kaunti ya Nyeri, Kenya, Aprili 26, 2021. (Picha na Charles Onyango/Xinhua)

Nyaguthii anaweza kupata popote kati ya shilingi 500 za Kenya (kama dola 3.8 za Kimarekani) hadi dola za Kimarekani 7.7 kwa siku kutoka kwenye mradi huo. "Hii ni bora zaidi ikilinganishwa na dola 2.3 nilizorudi nazo nyumbani kutokana na kazi duni na zisizotegemewa katika mashamba ya watu," amesema Nyaguthii katika mahojiano ya hivi karibuni na Shirika la Habari la China, Xinhua.

Yeye ni miongoni mwa wanawake zaidi ya 300 waliopata faraja katika eneo la Rukandu, mojawapo ya masoko mengi ya muda ambayo yamejitokeza kando ya sehemu ya barabara yenye urefu wa kilomita 84 inayojengwa karibu na makutano ya Marua, na maelfu ya wengine pia wanapata pesa katika eneo hilo vivyo hivyo kwenye barabara yenye shughuli nyingi.

Wanauza mazao ya shambani kama vile mshale, mihogo, viazi vitamu na matunda, biashara ambayo inawawezesha watu wengi wenye kipato cha chini kwa mtaji mdogo tu.

Mradi huo unasimamiwa na Mamlaka ya Taifa ya Barabara Kuu ya Kenya, na unafadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 69, Afrika Kukua Pamoja kwa asilimia 12, na serikali ya Kenya kwa asilimia 19, na utagharimu dola za Kimarekani jumla ya milioni 273.3.

Kwa mujibu wa tovuti ya Kundi la AfDB, muda wa jumla wa utekelezaji wa mradi huo ni miaka mitano kuanzia Mwaka 2020 hadi 2025.

Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Mei 2022, ikionyesha sehemu ya Barabara kuu ya Nairobi, Kenya. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa tarehe 8 Mei 2022, ikionyesha sehemu ya Barabara kuu ya Nairobi, Kenya. (Xinhua/Dong Jianghui)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha