超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Donald Trump, Kamala Harris wakubali kufanya mdahalo wa Septemba 10 kwenye Kituo cha Utangazaji cha ABC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2024

Picha ya iliyounganishwa pamoja ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump (kushoto) na Makamu wa Rais Kamala Harris. (Xinhua)

Picha ya iliyounganishwa pamoja ya Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump (kushoto) na Makamu wa Rais Kamala Harris. (Xinhua)

NEW YORK - Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump na Makamu wa Rais wa sasa Kamala Harris wamekubali kufanya mdahalo wa Septemba 10 kupitia Kituo cha Utangazaji cha ABC, kituo hicho kimethibitisha siku ya Alhamisi katika taarifa yake, ambapo kimesema Trump, mgombea wa urais wa Chama cha Republican, na Harris, mgombea wa Chama cha Democrat, wamethibitisha ushiriki wao katika mdahalo huo.

Mdahalo huo wa dakika 90 unatarajiwa kufanyika Philadelphia, na watangazaji wa ABC David Muir na Linsey Davis watakuwa waongozaji wa mdahalo huo, kwa mujibu wa gazeti la New York Times.

Mdahalo huo pengine utafanyika bila hadhira ya moja kwa moja, lakini muundo na kanuni hasa za msingi bado hazijaamuliwa, taarifa hiyo imesema, ikinukuu watu wawili wanaojua mipango hiyo.

Tangazo hilo linafuatia mkutano wa Trump na wanahabari huko Palm Beach, Florida, ambapo alipendekeza kufanya midahalo mitatu na Harris. Hapo awali Trump alikubali kufanya mdahalo na Rais Joe Biden Septemba 10, lakini akajiondoa baada ya Biden kujiondoa kwenye kugombea urais.

Trump pia amesema kwamba atafanya midahalo na Harris katika awamu zingine mbili, katika mdahalo utakaoandaliwa na vituo vya televisheni vya NBC na Fox. Lakini timu ya kampeni ya Harris haijakubaliana na midahalo hiyo, ambayo haikuwa sehemu ya ratiba ya awali ya midahalo ambayo Biden na Trump walikuwa wamekubaliana mwezi Mei.

Kwenye mdahalo wa awali wa mwaka huu mwezi Juni, uwezo wenye kuyumba na kupungua wa Biden ulizua hofu miongoni mwa wanachama wa Chama cha Democrat hali ambayo hatimaye ilipelekea rais kuachia nafasi yake ya kuwa mgombea wa chama chake.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha