超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji yatangaza mpangilio wa vyama kwenye karatasi ya kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa Oktoba

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2024

Picha hii iliyopigwa tarehe 29 Julai 2023, ikionyesha mandhari ya ufukwe mjini Maputo, Msumbiji. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa tarehe 29 Julai 2023, ikionyesha mandhari ya ufukwe mjini Maputo, Msumbiji. (Xinhua/Dong Jianghui)

MAPUTO - Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Msumbiji (CNE) imetangaza mpangilio wa vyama vya siasa kwenye karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa Oktoba, huku chama cha Vuguvugu la Kidemokrasia la Msumbiji (MDM) kikipangwa nafasi ya kwanza, chama tawala cha FRELIMO kikiwekwa nafasi ya pili, na chama kikuu cha upinzani, RENAMO kikiwa nafasi ya tatu.

Mbali na mpangilio huo wa vyama kwenye karatasi ya kupigia kura, Rodrigues Timba, mratibu wa masuala ya sheria na maadili wa CNE, pia ametoa ratiba ya mgao wa muda wa vyama vya siasa katika kujinadi kwenye vyombo vya habari vya umma.

Picha hii iliyopigwa tarehe 27 Julai 2023, ikionyesha mandhari ya Mji wa Maputo, Msumbiji. (Xinhua/Dong Jianghui)

Picha hii iliyopigwa tarehe 27 Julai 2023, ikionyesha mandhari ya Mji wa Maputo, Msumbiji. (Xinhua/Dong Jianghui)

Timba alisema kwenye mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne mjini Maputo, mji mkuu wa Msumbiji, kuwa muda huo wa kujinadi kwa vyama utakuwa wa kila wiki na wa zamu, siyo tu kwa vyama vitatu bungeni lakini pia kwa vyama vingine visivyo na wabunge vinavyoshiriki uchaguzi huo.

Tangazo hilo la mpangilio wa nafasi za vyama linakuja kufuatia uamuzi wa Baraza la Katiba uliotolewa hivi karibuni kuondoa Muungano wa Ushirikiano wa Kidemokrasia (CAD) kutoka kwenye Uchaguzi wa Wabunge, wa Mabaraza ya Majimbo na wa Magavana wa Majimbo. Kiongozi wa CAD Venancio Mondlane pekee ndiye amebaki kuwa mgombea wa urais.

Paulo Cuinica, Msemaji wa CNE, amesema kuwa kampeni za uchaguzi zitaanza Agosti 24 na kuendelea hadi Oktoba 6, 2024, zikihitaji jumla ya kiasi cha meticais milioni 240 za Msumbiji (karibu dola milioni 3.8 za Kimarekani).

Sehemu kubwa ya kiasi hiki, kama itapatikana, itatengwa kwa vyama vya siasa ili kusaidia kampeni zao, Cuinica amesema. "CNE inasubiri kulipwa kiasi hiki na Wizara ya Uchumi na Fedha."

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha