Lugha Nyingine
Msomi wa Nigeria: Ushirikiano kati ya China na Afrika waiwezesha Afrika kutimiza “Agenda ya Mwaka 2063”
Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha utafiti wa Nigeria katika Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang Dkt. Michael Ehizuelen amesema, ushirikiano wa karibu wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika unaiwezesha Afrika kutimiza “Agenda ya 2063”, na kuchangia katika ustawi wa pamoja.
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Wizara ya Mambo ya Nje ya China zimeonesha kuwa, thamani ya biashara kati ya China na Afrika katika mwaka 2023 ilifikia dola za kimarekani bilioni 182.1, na kuifanya China iendelee kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo. Dkt. Ehizuelen amesema, Afrika bado iko nyuma katika ushindani wa mnyororo wa thamani duniani kutokana na ukosefu wa teknolojia na ujuzi vinavyohitajika katika kuongeza thamani ya bidhaa. Lakini kwa upande mwingine, Afrika ina utajiri mkubwa wa maliasili na nguvukazi, kwa hiyo inahitaji uwekezaji na uungaji mkono kutoka kwa China, ili kuongeza tija na ufanisi katika uzalishaji mali.
Dkt. Ehizuelen amesema, ushirikiano kati ya Afrika na China unatoa msukumo kwa juhudi za Afrika kuelekea Agenda ya Mwaka 2063, na kwamba wakati agenda hiyo itakapotimizwa, hakika Afrika itaboresha nafasi yake katika mnyororo wa thamani duniani na kupunguza urari mbaya katika biashara ya kimataifa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma