Lugha Nyingine
China na Marekani zaanza mazungumzo ya duru mpya ya kimkakati mjini Beijing
Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya nje ya Kamati kuu ya Chama, akifanya mazungumzo ya duru mpya ya kimkakati kati yake na Jake Sullivan, msaidizi wa rais wa Marekani anayeshughulikia mambo ya usalama wa nchi hapa Beijing, China, Agosti 27, 2024. (Xinhua/Ding Lin)
Wang Yi, mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na mkurugenzi wa Ofisi ya mambo ya nje ya Kamati kuu ya Chama na Jake Sullivan, msaidizi wa rais wa Marekani wa mambo ya usalama wa nchi walianza mazungumzo ya duru mpya ya kimkakati Agosti 27 hapa Beijing.
Wang Yi alisema, anamkaribisha Sullivan kuja China kwa mara ya kwanza kufanya mazungumzo ya kimkakati kati ya China na Marekani. Uhusiano kati ya China na Marekani unahusiana na nchi hizo mbili zenyewe, lakini unafuatiliwa na dunia nzima. Katika miaka ya hivi karibuni iliyopita, uhusiano wa nchi hizo mbili ulikabiliwa na matatizo mengi. Kutokana na uelekezaji wa kimkakati wa rais Xi Jinping na rais Joe Biden, tumetimiza lengo la “Kurejea kwenye makubaliano yaliyofikiwa Kisiwa Bali na Kuelekea makubaliano yaliyofikiwa San Francisco”, ambapo tumepata maarifa muhimu, na mafunzo pia, ambayo tunatakiwa kukumbuka, na muhimu zaidi ni kushikilia mwelekeo mkuu wa kuheshimiana, kuishi pamoja kwa amani na kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja.
Kwa upande wake Sullivan alisema, hii ni mara yake ya kwanza kutembelea China akiwa msaidizi wa rais wa mambo ya usalama wa nchi, na aliushukuru upande wa China kwa mapokezi mazuri. Alisema, Rais Biden anajikita kwa kuwajibika katika kusimamia uhusiano kati ya Marekani na China, kuepusha ushindani kubadilika kuwa mgogoro, na kufanya ushirikiano katika sekta zenye maslahi ya pamoja. Anatarajia kwa kupitia mawasiliano ya kimkakati, atafanya mazungumzo yenye mafanikio pamoja na upande wa China juu ya masuala mengi mbalimbali, na kutekeleza vizuri makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa nchi hizi mbili.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma