超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Xi akutana na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika

(CRI Online) Septemba 04, 2024

Asubuhi ya tarehe 3, Septemba, rais Xi Jinping wa China akikutana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika 2024. (Picha na Huang Jingwen/Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China tarehe 3 amekutana na Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat, ambaye yuko Beijing kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024.

Akibainisha kuwa Umoja wa Afrika ni bendera inayoongoza umoja na uimarishaji wa Afrika na jukwaa muhimu la ushirikiano wa kimataifa, Rais Xi amesema China inaunga mkono Umoja huo kuchukua nafasi kubwa zaidi katika maendeleo ya urafiki kati ya China na Afrika.

Amesema China iko tayari kutafuta mafanikio makubwa katika sekta mbalimbali katika ushirikiano wake na Umoja wa Afrika na kuinua jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja hadi kufikia ngazi mpya.

Rais Xi amesisitiza kuwa China inaichukulia Afrika kuwa kipaumbele kikuu katika mambo yake ya diplomasia, na inapenda kuongeza mawasiliano ya kisiasa, kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati na ushirikiano wa kivitendo, kubadilishana uzoefu wa maendeleo na kukuza maendeleo kwa pamoja na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha