Lugha Nyingine
China kufanya mkutano wa ngazi ya juu wa IP kwa nchi za BRI
Roboti zikisalimiana kwenye Mkutano wa Dunia wa Roboti 2024 mjini Beijing, China, Agosti 21, 2024. (Xinhua/Jin Liwang)
BEIJING - China imepanga kufanya Mkutano wa Tatu wa Ngazi ya Juu kuhusu Haki Miliki kwa Nchi zilizo kando ya "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuanzia Septemba 11 hadi 13 mjini Beijing, Mamlaka ya kitaifa ya Hakimiliki ya China (CNIPA) imesema siku ya Jumatano.
Mkutano huo utaalika wakuu kutoka taasisi takriban 70 za IP za nchi zinazoshiriki ushirikiano wa Ukanda Mmoja, Njia Moja (BRI), pamoja na mashirika ya kimataifa na ya kikanda, kwa mujibu wa CNIPA.
Mkutano huo pia utaalika wawakilishi wa balozi mbalimbali nchini China, maafisa kutoka idara husika za China, wataalamu na wasomi, huku unatarajia kuhudhuriwa na washiriki takriban 450, CNIPA imesema.
Washiriki hao watajadili kwa kina ushirikiano wa kikanda, maendeleo ya kijani, kubadilisha muundo wake kuwa kidijitali na kuboresha thamani ya haki miliki, afisa mkuu wa CNIPA Sheng Li amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari.
Sheng ameongeza kuwa, katika mkutano huo wa siku tatu, CNIPA, Shirika la Dunia la Haki Miliki na Ofisi ya Hakimiliki ya Eurasian zitaandaa mikutano kujadili mada zinazohusiana na mchango wa IP katika kuendesha maendeleo bunifu ya kampuni.
China imehimiza kikamilifu mawasiliano na ushirikiano na nchi washirika wa BRI katika nyanja mbalimbali, zikiwemo sera za IP, mafunzo kwa watu wenye ujuzi, elimu na mitihani.
Imetia saini mikataba ya ushirikiano wa IP na nchi 57 washirika wa BRI. Tangu Mwaka 2013, China imeendesha kozi zaidi ya 50 za mafunzo, na kuwaandaa watu zaidi ya 1,300 wenye ujuzi wa haki miliki kutoka nchi hizo.
Wataalamu wa China pia wametumwa kwa nchi na mashirika ya kimataifa zaidi ya 10 kufanya mawasiliano na mafunzo, kuunga mkono ujenzi wa uwezo wa IP kwa nchi washirika wa BRI.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma