Lugha Nyingine
China na Brazil zaamua kuinua uhusiano kwenye jumuiya yenye mustakabali wa pamoja
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakifanya mazungumzo huko Brasilia, Brazil asubuhi ya tarehe 20, Novemba. (Xinhua)
China na Brazil zimeamua kuinua uhusiano wao kwenye jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kwa ajili ya dunia yenye haki zaidi na sayari endelevu zaidi.
Uamuzi huo umetolewa wakati wa mkutano kati ya Rais Xi Jinping wa China ambaye yupo kwenye ziara ya kiserikali nchini humo baada ya kuhudhuria mkutano wa 19 wa G20 mjini Rio de Janeiro, na mwenzake wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva.
Xi amefafanua kuwa uhusiano wa China na Brazil uko katika kiwango bora zaidi katika historia, ambao sio tu umeboresha ustawi wa watu wa nchi hizo mbili, bali pia umetetea maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, umeimarisha nguvu na sauti ya nchi za Kusini, na kutoa mchango mkubwa kwa amani na utulivu duniani. Aidha alisema kuwa China na Brazil pia zimeamua kuunganisha Mpango wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” na mikakati ya maendeleo ya Brazil.
Kwa upande wake Lula amesema Brazil na China ni marafiki wazuri wanaoheshimiana na kutegemeana, China ni mshirika muhimu wa kimkakati wa Brazil, na watu wa China ni marafiki wa kutegemewa wa watu wa Brazil.
Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva wakifanya mazungumzo huko Brasilia, Brazil asubuhi ya tarehe 20, Novemba. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma