超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Rais Xi Jinping wa China atoa wito wa kuendeleza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati na Nepal

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 04, 2024

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai  la Beijing, Desemba 3, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa la Diaoyutai la Beijing, Desemba 3, 2024. (Xinhua/Yao Dawei)

BEIJING - Rais wa China Xi Jinping amekutana na Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli mjini Beijing siku ya Jumanne, akiahidi kufanya juhudi za kuendeleza uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati na Nepal huku akisifu dhamira thabiti ya muda mrefu aliyonayo Oli kwa kuhimiza urafiki kati ya pande hizo mbili.

Rais Xi amesema China na Nepal zinaunganishwa kwa milima na mito, nchi hizi mbili ni majirani wema, marafiki wazuri na washirika wazuri, na uhusiano wa pande mbili umedumisha maendeleo mazuri na tulivu.

Akibainisha Rais Xi amesema kuwa mwaka ujao ni maadhimisho ya miaka 70 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia, China inaiweka Nepal kwenye nafasi muhimu katika mambo yake ya diplomasia ya ujirani mwema, na inapenda kushirikiana na Nepal katika kuimarisha urafiki wao wa jadi na kusukuma mbele maendeleo mapya ya uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Nepal ulio wa urafiki wa kudumu, maendeleo na ustawi.

Rais Xi akisisitiza kuwa China inaheshimu chaguo la Nepal kufuata njia ya maendeleo inayolingana na hali halisi ya nchi yake, inaiunga mkono Nepal katika kulinda uhuru, mamlaka ya nchi na ukamilifu wa ardhi. "China inapenda kushirikiana na Nepal katika kuimarisha hali ya kuaminiana kimkakati na kutoa uungaji mkono thabiti katika masuala yanayohusiana na maslahi ya msingi ya kila upande.

Rais Xi ameeleza kuwa, China inapenda kuzidisha ushirikiano wa manufaa halisi na Nepal, kufanya ujenzi wa pamoja wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja, na kuimarisha ushirikiano katika nyanja kama vile bandari, uchukuzi, gridi za umeme na mawasiliano ya habari.

“China inapenda kuendelea kutoa msaada kwa iwezekanavyo kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya Nepal, na kuzitia moyo kampuni za China kuwekeza na kufanya biashara nchini Nepal,” Rais Xi amesema.

China inapenda kuimarisha uratibu na Nepal ndani ya majukwaa ya kimataifa kama vile Umoja wa Mataifa, ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea, Rais Xi amesema.

Sharma Oli amesema kuwa hakuna matatizo kati ya China na Nepal, bali ni urafiki tu, ameishukuru China kwa kutoa uungaji mkono mbalimbali wa thamani kwa Nepal, na Nepal inakaribisha kampuni zaidi za China kuwekeza nchini humo na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Oli amesema, Xizang na Taiwan zote ni sehemu zisizoweza kutengwa za ardhi ya China, akisisitiza kwamba Nepal inafuata kithabiti kanuni ya kuwepo kwa China moja, na inapinga uingiliaji wa nchi yoyote kati ya mambo ya ndani ya China.

Taarifa ya pamoja ya Jamhuri ya Watu wa China na Nepal pia imetolewa siku hiyo ya Jumanne.?

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa Diaoyutai  la Beijing, Desemba 3, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

Rais wa China Xi Jinping akikutana na Waziri Mkuu wa Nepal KP Sharma Oli, ambaye yuko katika ziara rasmi nchini China, kwenye Jumba la Wageni wa Kitaifa Diaoyutai la Beijing, Desemba 3, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha