超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Mkutano wa kimataifa wa ukusanyaji wa fedha za mambo ya Tabianchi wafunguliwa kusini mwa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 09, 2024

GUANGZHOU - Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji na Ukusanyaji wa Fedha za Mambo ya Tabianchi wa Ghuba ya Pearl 2024, wenye mada kuhusu ushirikiano wa kimataifa na mustakabali wa kijani, umefunguliwa jana Jumapili huko Guangzhou, mji mkubwa wa kusini mwa China.

Akitoa hotuba kwenye mkutano huo, Liu Jian, naibu mkuu wa Xinhua, Shirika la Habari la China, amesisitiza kwamba Xinhua likiwa shirika la habari la serikali ya China na shirika la habari la kimataifa, litatumia vya kutosha mfumo wake wa utangazaji wa kote duniani wa vyombo vyote vya habari na nguvu bora ya jumuiya ya washauri bingwa ya hali ya juu kufanya ushirikiano kwa karibu na pande zote duniani ili kuhimiza kwa pamoja ufikiaji wa malengo mawili ya hewa ya kaboni.

Meya wa mji wa Guangzhou Sun Zhiyang amesema katika hotuba yake kuwa mkutano huo una umuhimu mkubwa katika kuendeleza utekelezaji wa malengo mawili ya China ya hewa ya kaboni, kujenga China inayopendeza, vilevile kushughulikia mabadiliko ya tabianchi duniani.

Amesema Mji wa Guangzhou utaungana na nchi mbalimbali duniani na sekta zote za jamii ili kuhimiza kwa pamoja maendeleo makubwa katika uwekezaji na ukusanyaji wa fedha za mambo ya tabianchi.

Zhao Yingmin, naibu waziri wa ikolojia na mazingira wa China, ameeleza kuwa uwekezaji na ukusanyaji wa fedha za mambo ya tabianchi ni sehemu muhimu ya mambo ya fedha ya kijani.

“Kuongoza na kuhamasisha mitaji zaidi ya kijamii ili kuunga mkono uvumbuzi wa teknolojia ya kijani ya kutoa kaboni chache na kubadilisha muundo wa viwanda kunaweza kuleta matokeo yenye ufanisi kwa tabianchi, jamii na uchumi, na pia kuongeza msukumo mpya na njia mpya kwa maendeleo yenye ubora wa juu," Zhao ameongeza.

Mkutano huo wa siku mbili umeandaliwa kwa pamoja na ofisi ya kazi ya chapa ya Shirika la Xinhua na tawi la Guangdong la shirika hilo, pamoja na Shirika la Upashanaji Habari za Kiuchumi la China.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha