Lugha Nyingine
Madaktari wa China watoa huduma bila malipo katika kuadhimisha Siku ya Kunawa Mikono
(Picha inatoka tovuti ya CRI)
Timu ya wataalam wa matibabu wa China imetoa elimu ya afya na huduma za matibabu bila malipo katika Visiwa vya Pemba nchini Tanzania ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Kunawa Mikono Duniani mwaka huu.
Shughuli hiyo iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Kiwani na Kitengo cha Zahanati ya Afya ya Msingi, iliongozwa na kundi la pili la wataalam wa Mradi wa Msaada wa Kudhibiti na Kutokomeza Ugonjwa wa Kichocho kutoka China na Zanzibar na Kundi la 34 la Timu ya Madaktari wa China iliyopo Pemba.
Huduma hiyo, ambayo imevutia wakazi na wanafunzi wenyeji zaidi ya 400, imefanywa kwa ushirikiano na wawakilishi kutoka idara za afya na elimu na Kitengo cha Programu ya Magonjwa ya Kitropiki Yaliyosahaulika (NTD) visiwani Zanzibar.
(Picha inatoka tovuti ya CRI)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma