Treni zinazosafiri kati ya China na nchi za nje, shughuli za biashara zenye pilikapilika, na bidhaa za aina mbalimbali.
Wakati usiku unapoanza na taa kuwashwa, gulio kubwa la kimataifa la mkoani Xinjiang, China hujaa watu wengi na kuonesha hali motomoto. Kwenye Mtaa wa chakula wa Gulio Kubwa la Kimataifa la Xinjiang, China ukiwa umezungukwa na taa nzuri za mapambo, sauti za nyimbo za jadi za kabila la Wauygur zinasikika eneo zima, salamu za makaribisho ya wauzaji na mazungumzo ya wateja ni kila mahali, na nyama choma ya mbuzi, kuku pilipili na vyakula vingine mbalimbali vinaonesha picha ya maisha ya usiku ya mji yenye hali motomoto, yakivutia watalii wengi kutoka ndani na nje ya China kwenda huko kutembelea soko hilo la usiku, kuonja chakula kitamu na kujionea uzuri wa Xinjiang.
Takwimu zinaonesha kuwa, mawigi sita kati ya kila mawigi kumi ya nywele yanatoka Xuchang, Mkoa wa Henan wa China, ambao pia unajulikana kwa jina la “Mji Mkuu wa Mawigi Duniani.” Mawigi yanayozalishwa na Kampuni inayojulikana sana ya Rebecca siyo tu ni maarufu sana nchini China, bali pia katika masoko ya nje ya China, hasa katika mabara ya Amerika na Afrika.
Ni kwa namna gani kipande cha chuma kinageuka kuwa gari zima? Kiwanda cha Kampuni ya Magari ya BYD kilichopo mji wa Zhengzhou wa Mkoa wa Henan, China kiko hapa kujibu maswali yako. Hebu tuingie ndani ya kiwanda hicho pamoja na timu ya utafiti ya waandishi habari wa People’s Daily Online ya “China Inayosonga Mbele” na kutazama pamoja namna magari yanavyoundwa.