Lugha Nyingine
Maono ya Rais Xi juu ya Kujenga Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja
Beijing - Rais wa China Xi Jinping Jumatatu hii kupitia njia ya video amehudhuria na kutoa hotuba ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Huku akiweka umuhimu mkubwa kwa uhusiano kati ya China na Afrika, Xi amekuwa akisisitiza mara kwa mara ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja. Yafuatayo ni baadhi ya mambo muhimu ya matamshi yake kuhusiana na hili.
Juni 21, 2021
Katika mazungumzo ya simu na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Xi alisema kuwa China iko tayari kujiunga na Tanzania katika kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kuongeza uungaji mkono wa pande zote, kulinda kwa pamoja haki halali na maslahi ya nchi zinazoendelea, na kutoa mchango wenye hamasa katika ujenzi wa jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Juni 17, 2020
"Katika kukabiliana na janga la UVIKO-19, China na Afrika zimesaidiana na kupigana bega kwa bega," Xi alisema katika Mkutano Maalum wa China na Afrika kuhusu Mshikamano dhidi ya UVIKO-19.
"Katika kukabiliana na UVIKO-19, China na Afrika zimeimarisha mshikamano na kuimarisha urafiki na kuaminiana," Xi aliongeza.
"Kuisaidia Afrika kupata maendeleo endelevu ndiyo jambo la msingi katika siku zijazo. China inaunga mkono Afrika katika jitihada zake za kuendeleza eneo la Biashara Huru la Bara la Afrika na kuboresha mawasiliano na kuimarisha minyororo ya viwanda na ugavi. China itatafuta ushirikiano mpana na Afrika katika mambo mapya kama uchumi wa kidijitali, kujenga miji ya kisasa, nishati safi, na teknolojia ya 5G ili kukuza maendeleo na ufufukaji wa uchumi wa Afrika," alisema.
Juni 25, 2019
Katika barua ya pongezi kwa ufunguzi wa Mkutano wa Waratibu wa Utekelezaji wa Hatua za Ufuatiliaji wa Mkutano wa Kilele wa FOCAC wa Beijing, Xi alisema, Mkutano wa FOCAC wa Beijing ni hatua muhimu katika historia ya uhusiano kati ya China na Afrika.
Alisema anatumai pande hizo mbili zitazingatia kanuni ya mashauriano na ushirikiano kwa manufaa ya pamoja, kuimarisha mawasiliano na harambee, kuzidisha mshikamano na ushirikiano, na kupiga hatua thabiti katika kusukuma mbele utekelezaji wa mafanikio ya mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing na ujenzi wa pamoja wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".
Aliongeza kusema, kwa kufanya hivyo, pande hizo mbili zinaweza kuendelea kuboresha ustawi wa watu bilioni 2.6 nchini China na Afrika na kufanya juhudi zisizo na kikomo za kujenga jumuiya ya uhusiano wa karibu zaidi kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja.
Septemba 3, 2018
Akihutubia kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa FOCAC wa Mwaka 2018 uliofanyika Beijing, Xi alisema, "Pamoja na mikosi inayofanana katika siku za nyuma na dhamira ya pamoja, China na Afrika zimeonesha kuhurumiana na kusaidiana kwa miaka yote. Kwa pamoja, tumeanza njia ya kipekee ya ushirikiano wa kunufaishana.
"Tukitembea katika njia hii, China imefuata kanuni ya ukweli, matokeo ya kweli, upendo na imani nzuri na kanuni ya kutafuta maslahi makubwa zaidi na ya pamoja. China imesimama na nchi za Afrika. Kwa pamoja tumefanya kazi kwa umoja na kusonga mbele" Xi alisema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma