Lugha Nyingine
Sherehe ya kipekee yafanyika kwa ajili ya Mwaka Mpya ujao wa Jadi wa Tibet (2)
Watoto wakicheza kwenye sherehe katika duka la vitabu mjini Lhasa, Mkoa unaojiendesha wa Xizang, Kusini-Magharibi mwa China, Februari 3, 2024. (Picha na Tenzin Nyida/Xinhua) |
Sherehe ya kipekee imefanyika siku ya Jumamosi katika duka la vitabu vya watoto katika Mji wa Lhasa, ambapo walimu walitambulisha na kufahamisha mila na desturi za kijadi za Mwaka Mpya wa Jadi wa Tibet. Kwenye sherehe hiyo, watoto waliovalia mavazi ya kijadi ya Kitibet walifurahia maonyesho ya muziki, maonyesho ya vikaragosi na utengenezaji wa kazi za mikono, pamoja na karamu ya "gutu", chakula cha kijadi cha supu kinachotengenezwa kwa unga wa ngano.
Katika picha: Ndege yangeyange wakiwa wamepumzika kwenye Ziwa Yundang huko Xiamen China
Picha: Mandhari ya Ziwa Yundang la Xiamen, China katika ukungu
Picha:Majengo Makongwe katika Kisiwa cha Kulangsu, China ambayo yanabeba ushuhuda wa historia
Mandhari ya kushangaza ya “Barabara Kuu inayoning’inia kwenye Miteremko ya Vilima” wakati wa theluji
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma