Lugha Nyingine
Sherehe ya "Kuonyesha Buddha" yafanyika katika Hekalu Kaskazini Magharibi mwa China (5)
LANZHOU - Waumini na watalii zaidi ya 40,000 kutoka ndani na nje ya China wamehudhuria sherehe kubwa ya Wabuddha wa Tibet, inayojulikana kama sherehe ya "Kuonyesha Buddha", iliyofanyika Alhamisi kwenye Hekalu la Labrang katika Mkoa wa Gansu nchini China ambapo takriban lama 100 walibeba kitambaa kikubwa cha Thangka chenye picha ya Buddha kutoka jumba la maandiko hadi kilima kilicho karibu, wakifuatiwa na waumini wa Dini ya Buddha pamoja na watalii.
Thangka hiyo ilioneshwa kwa umma majira ya saa 5 Asubuhi kwenye kilima kwa ajili ya waumini kuabudu. Waumini na watalii waliwasilisha hada, au mitandio myeupe ya sherehe, mbele ya Thangka hiyo ili kuomba baraka na bahati njema.
Tukio hilo liliisha baada ya nusu saa.
Zhou Guangping, mpenda upigaji picha kutoka Mkoa wa Guangdong Kusini mwa China, alishiriki kwenye sherehe hiyo.
"Baada ya kusikia marafiki zangu wakizungumza kuhusu shughuli ya kuvutia la 'kuonyesha Buddha' katika Hekalu la Labrang, nilifunga safari hapa ili kurekodi siku hii muhimu kwa kamera yangu, kupata uzoefu wa utamaduni wa watu wa Tibet, na ninatumaini kwamba itaipatia familia yangu usalama na furaha," Zhou amesema.
Shughuli hiyo ya kila mwaka ni moja ya sherehe muhimu zaidi katika Hekalu la Labrang, mojawapo ya mahekalu sita makubwa ya Madhehebu ya Gelug ya Wabuddha wa Tibet. Hekalu hilo lilijengwa Mwaka 1709 na linatumika kama taasisi ya juu ya elimu ya Ubuddha wa Tibet nchini China.
Tukio hilo hufanyika kila mwaka siku ya 13 ya mwezi wa kwanza wa kalenda ya kilimo ya China. Siyo tu sikukuu kubwa kwa Wabudha, lakini pia jukwaa la kuonyesha utamaduni na desturi za kipekee za Tibet kwa watalii.?
Watu wa kabila la Wagelao washerehekea Sikukuu ya Maolong huko Guizhou, Kusini Magharibi mwa China
Wakulima kote China wawa na pilika nyingi za uzalishaji wa kilimo wakati Siku ya Yushui yakiwadia
Ndege C919 ya China yashiriki mazoezi ya Maonyesho ya Anga ya Singapore
Chuo Kikuu cha Kenyatta chafanya maonyesho ya dragoni wa China ili kukuza mawasiliano ya kitamaduni
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma