Lugha Nyingine
Xi Jinping akagua kazi ya kilimo cha majira ya mchipuko (2)
CHANGSHA - Rais Xi Jinping wa China, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) ameingia na kutembea shambani kukagua kilimo cha majira ya mchipuko na maandalizi yake wakati wa kufanya ukaguzi katika Mji wa Changde, Mkoa wa Hunan, katikati ya China siku ya Jumanne.
Kilimo bora cha majira ya mchipuko na maandalizi yake ni muhimu katika kuhakikisha mavuno ya nafaka na usalama wa chakula, Rais Xi amesema.
Mikoa yote na idara zote zinapaswa kubaini wajibu wao, kuhakikisha eneo la kutosha kwa ajili ya upandaji mazao wa majira ya mchipuko, kupanga vema usimamizi wa mashamba ya kilimo cha majira ya mchipuko, ili kuhakikisha utoaji wa kutosha wa mazao ya kilimo na kuimarisha huduma za kilimo za kijamii, Rais Xi amesisitiza.
Ametoa wito wa kuimarishwa kwa juhudi za kuzidisha mafungamano ya mbegu zenye sifa bora, mbinu za kilimo, mashine za kilimo na mashamba.
Sera za kuunga mkono kilimo na wakulima zinapaswa kutekelezwa ipasavyo ili kuhakikisha mapato ya wakulima wa nafaka na kuwachochea kupanda nafaka ili kupata mwanzo mzuri wa kuongeza pato la nafaka na mapato ya wakulima kwa mwaka mzima, Rais Xi amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma