Lugha Nyingine
Wanaanga?wa China wa Chombo cha Shenzhou-18 wakamilisha kazi yao ya?kwanza ya kutembea kwenye anga ya juu
BEIJING – Wanaanga wa China wa chombo cha anga ya juu cha Shenzhou-18 walioko kwenye kituo cha anga ya juu cha China wamekamilisha kazi yao ya kwanza ya kutembea kwenye anga ya juu saa 12:58 jioni (Kwa saa za Beijing) siku ya Jumanne, Shirika la Anga ya Juu la China (CMSA) limesema.
Ye Guangfu, Li Cong na Li Guangsu wamefanya kazi kwa saa takriban nane na nusu katika kukamilisha majukumu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ufungaji wa vifaa vya kulinda vifusi angani, na wamesaidiwa na mkono wa roboti wa kituo hicho na timu iliyoko duniani.
Jukumu hilo limeweka rekodi mpya kwa kuwa kutembea kwenye anga ya juu kwa muda mrefu zaidi kwa mara moja kuwahi kufanywa na wanaanga wa China.
Ye na Li Guangsu, wanaanga wawili waliopewa jukumu hilo la kutembea kwenye anga ya juu, wamerejea salama kwenye chombo cha maabara cha Wentian.
Hii ni mara ya pili kwa Ye kufanya shughuli ya nje ya chombo, kufuatia kutembea kwenye anga ya juu wakati wa ujumbe wa chombo cha Shenzhou-13, huku Li Guangsu akitembea kwenye anga ya juu kwa mara ya kwanza.
Ujumbe wa wanaanga hao utahusika na majukumu mengine mengi, huku wanaanga wa Shenzhou-18 wakiwa wamejipanga kushiriki katika majaribio kadhaa ya sayansi ya anga ya juu na majaribio ya kiufundi, wakati pia watafanya shughuli za nje ya chombo cha anga ya juu za nyongeza na kufunga mizigo nje ya kituo cha anga ya juu, CMSA imesema.
Hadi kufikia sasa, wanaanga wa China wamefaulu kutekeleza jumla ya shughuli za nje ya chombo 16. Septemba 27, 2008, mwanaanga Zhai Zhigang katika ujumbe wa Shenzhou-7 aliweka historia ya kuwa mtu wa kwanza wa China kutembea kwenye anga ya juu, ambayo yaliendelea kwa dakika takriban 19.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma