Lugha Nyingine
Timu ya China yaandaa darasa la ulinzi wa mabaki ya kale ya kitamaduni kwa wanafunzi wa Afghanistan
BAMIYAN, Afghanistan – Masomo ya nje ya darasa yaliyoandaliwa na timu ya watu sita inayoundwa na wataalam wa utafiti wa mabaki ya kale na mali ya urithi wa kitamaduni wa China, pamoja na wataalam na maofisa wa Afghanistan yalifanyika kwenye eneo kubwa la Waumini wa Imani wa Kibuddha na Shahr-e Gholghola, yote yakiwa ni maeneo ya mali ya urithi ya Dunia yaliyoorodheshwa na UNESCO katika Bonde la Bamiyan. Masomo hayo yanayolenga kuongeza uelewa wa ulinzi wa mabaki ya kale ya kitamaduni kwa wanafunzi wa shule ya msingi wa Afghanistan yameanza siku ya Jumapili katikati mwa Jimbo la Bamiyan nchini Afghanistan.
Katika masomo hayo ya nje ya darasa, wanafunzi wa Afghanistan walifundishwa kuhusu hali ilivyo sasa ya ulinzi wa mabaki ya kale ya kitamaduni huko Bamiyan, ujuzi wa vitendo unaohitajika kwa ajili ya ulinzi wa mali hiyo ya urithi, na historia ya mawasiliano ya kitamaduni kati ya Afghanistan na China kwenye Njia ya kale ya Hariri.
"Nataka kuchangia maendeleo ya baadaye ya nchi yangu na kufanya kazi katika Nyanja ya historia na akiolojia katika siku zijazo," amesema Mohammad Zaid, mwanafunzi wa darasa la sita katika masomo hayo ya nje ya darasa, ambaye alipokea cheti kwa ufaulu wake mzuri.
Jimbo la Bamiyan nchini humo inajivunia maeneo kadhaa ya mabaki ya kale ya kitamaduni, zikiwemo sanamu mbili za Buddha ambazo zina umri wa zaidi ya miaka 1,400.?
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma