超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Mji wa Jinhua, Mashariki mwa China wahimiza urithi na maendeleo ya opera ya Wu (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 27, 2024
Mji wa Jinhua, Mashariki mwa China wahimiza urithi na maendeleo ya opera ya Wu
Wasanii wa kikundi cha kienyeji cha Opera ya Wu wakijiandaa kufanya onyesho katika Kijiji cha Zhengdian cha mji mdogo wa Lipu, Mji wa Jinhua, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Juni 25, 2024. (Xinhua/Xu Yu)

Opera ya Wu, ambayo pia inajulikana kwa jina la Opera ya Jinhua, ina historia ya miaka zaidi ya 500. Kwa mara ya kwanza ilikua maarufu katika Mji wa Jinhua na maeneo ya jirani, na ilipewa jina la Wuzhou, ambalo lilikuwa jina la mji huo wa Jinhua katika China ya kale.

Serikali za mitaa za Wilaya ya Jindong katika mji huo wa Jinhua zimekuwa zikitafuta njia bora za kuendeleza urithi na maendeleo ya opera hiyo ya kijadi.

Tangu Machi mwaka huu, mji mdogo wa Lipu katika Wilaya ya Jindong ya Mji wa Jinhua imekuwa ikiandaa maonyesho ya Opera ya Wu katika kumbi za maeneo hayo kila wikiendi, ikiwapa wanakijiji na wapenzi wa Opera ya Wu hali changamani ya kufurahia opera hiyo. Hadi sasa, maonyesho zaidi ya 40 yameshafanyika.

Kijiji cha Zhengdian ni mfano mzuri wa kuendeleza utalii wa kitamaduni wa vijijini. Shughuli kama vile maonyesho ya opera na masoko ya kitamaduni na ubunifu ziliandaliwa, katika juhudi za kutoa jukwaa la maonyesho ya Opera ya Wu na kazi za mikono za kienyeji kama vile michoro ya kubandika kwenye nguo, uchongaji wa tofu na michoro kwa sukari.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha