Lugha Nyingine
Droni za kubeba mizigo na ndege maalumu zatumika katika usafirishaji wa matunda ya plamu huko Chongqing, China (4)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 05, 2024
Matunda ya plamu yameingia msimu wa mavuno katika Wilaya ya Wushan, Mji wa Chongqing wa Kusini Magharibi mwa China. Mwaka huu mtindo mpya wa kutumia droni za kubeba mizigo na ndege maalumu za Kampuni ya Usafiri wa Anga ya Shirika la Posta la China umekuwa ukitumika katika usafirishaji wa matunda ya plamu ya wilaya hiyo. Matunda yaliyovunwa huweza kusafirishwa mara moja kutoka shambani hadi kiwanja cha ndege cha wilaya hiyo kwa kutumia droni za kubeba mizigo, na kisha kuchukuliwa na ndege maalumu mpaka Nanjing, Mkao wa Jiangsu wa Mashariki mwa China, kabla ya kusambazwa kwa wauzaji nchini kote China ndani ya saa 24. (Xinhua/Huang Wei)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma