超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Marais wa China na Guinea-Bissau wafanya mazungumzo na kuinua hadhi ya uhusiano wa pande mbili

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 11, 2024

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akipeana mkono na Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

BEIJING - China na Guinea-Bissau zemeinua hadhi ya uhusiano wao wa pande mbili siku ya Jumatano hadi kuwa uhusiano wa wenzi wa kimkakati, ambapo Rais wa China Xi Jinping na Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, wametangaza hatua hiyo wakati walipofanya mazungumzo mjini Beijing.

Akieleza kuwa katika miaka ya hivi karibuni, China na Guinea-Bissau zimezidisha uhusiano wa pande mbili, kuimarisha hali ya kuaminiana kisiasa, kupanua ushirikiano wa matokeo halisi na kuongeza uratibu wa kimataifa, Rais Xi amesema China inaiunga mkono Guinea-Bissau katika kutafuta kwa kujiamulia njia ya maendeleo inayolingana na hali halisi ya nchi yake.

Amesisitiza kuwa, China ingependa kuimarisha mawasiliano ya kirafiki na Guinea-Bissau kwenye ngazi zote, kubadilishana zaidi uzoefu katika masuala ya utawala, na kupanua ushirikiano katika sekta za kilimo, madini, ujenzi wa miundombinu na uchumi wa bluu chini ya mwongozo wa ujenzi wa kiwango cha juu wa Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Rais Xi amesema China inakaribisha mazao ya kilimo yenye ubora wa juu kutoka Guinea-Bissau kuingia katika soko la China, na kuhimiza kampuni za China kuwekeza na kufanya ushirikiano nchini Guinea-Bissau na kuisaidia Guinea-Bissau kubadilisha uwezo wake wa rasilimali kuwa nguvu ya maendeleo.

“China inapenda kuendelea kutoa uungaji mkono kwa iwezavyo kwa ujenzi wa ndani wa Guinea-Bissau, na itaendelea kutuma wataalam wake wa mpunga na timu za matibabu kusaidia Guinea-Bissau katika kuhakikisha usalama wa chakula na kuendeleza mambo ya afya ya umma,” ameongeza.

Rais Xi ametoa wito kwa pande hizo mbili kuimarisha mawasiliano na ushirikiano katika elimu, vijana na nyanja nyinginezo ili kuleta maelewano ya karibu ya watu wa nchi hizo mbili. Amesema China itaendelea kutoa ufadhili wa masomo wa kiserikali na fursa za mafunzo ili kuisaidia Guinea-Bissau kuwaandaa watu wengi zaidi wenye ujuzi kwa maendeleo ya nchi yake.

Rais Xi amesema Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ni jukwaa muhimu kwa watu wa China na Afrika kutekeleza Kanuni Tano za Kuishi Pamoja kwa Amani na kuhimiza maendeleo kwa pamoja.

Kwa upande wake Embalo amesema Guinea-Bissau na China zinafurahia uhusiano thabiti na wa kirafiki unaodhihirishwa na kuungana mkono kusikoyumbayumba, akiongeza kuwa kila Guinea-Bissau inapokabiliwa na matatizo, China siku zote inatoa msaada wenye thamani bila kusitasita, msimamo wake huo ambao watu wa Guinea-Bissau hawatausahau kamwe.

Embalo amesema Guinea-Bissau itaendelea kusimama kidete na China, kushikilia kanuni ya kuwepo kwa China moja na kuunga mkono msimamo wa China kuhusu maslahi yake ya msingi kama vile suala la Taiwan.

Rais Xi Jinping wa China akifanya mazungumzo hapa Beijing na Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye uwanja wa nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Ding Lin)

Rais Xi Jinping wa China akifanya hafla ya kumkaribisha Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, ambaye yuko katika ziara ya kiserikali nchini China, kwenye uwanja wa nje ya lango la mashariki la Jumba la Mikutano ya Umma kabla ya mazungumzo yao mjini Beijing, China, Julai 10, 2024. (Xinhua/Ding Haitao)

Rais Xi Jinping wa China na mkewe Peng Liyuan wakiwa katika picha ya pamoja na Umaro Sissoco Embalo, Rais wa Jamhuri ya Guinea-Bissau, na mkewe Dinisia Reis Embalo kabla ya mazungumzo kati ya Xi na Embalo mjini Beijing, China, Julai. 10, 2024. (Xinhua/Huang Jingwen)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha