Lugha Nyingine
Watafiti wa China wabuni saa ya mkononi inayopima hali ya afya kwa wakati halisi papo hapo kupitia jasho
Picha iliyopigwa Juni 20, 2024 ikionesha watafiti wakijaribu saa ya mkononi ya kupima hali ya afya kupita jasho huko Hefei, Mkoa wa Anhui wa China. (Xinhua/Qu Yan)
Wanasayansi kutoka Taasisi za Sayansi ya Fizikia za Hefei (HIPS) chini ya Akademia ya Sayansi ya China wamebuni saa ya mkononi inayoweza kupima kemikali muhimu kwenye jasho la mwili. Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa katika jarida la ACS Nano.
Jasho lina aina nyingi za madini muhimu, ambayo ni muhimu kwa kuunga mkono ufanyaji kazi wa misuli, neva za afya na mpigo wa kawaida wa moyo, amesema Yang Meng, profesa msaidizi katika taasisi hiyo na mmoja wa waandishi wa utafiti huo.
Saa hiyo ya mkononi iliyobuniwa na timu ya Yang hukusanya jasho kutoka kwenye ngozi na kulichambua katika wakati halisi papo hapo kwa kutumia chipu ya kuhisi.
Ingawa si wa kwanza kuvumbua chipu ya aina hiyo, watafiti hao wa China wamewekea mkazo skrini imara kwa ajili kufanya kazi kwa kuaminika kwa muda mrefu.
"Inazidi uthabiti wa vihisi jasho vingine vingi kwa kufuatilia kwa uendelevu ayoni za aina tatu kwenye jasho la binadamu kwa zaidi ya miezi sita," amesema mtafiti mkuu Huang Xingjiu kutoka Taasisi ya Fizikia ya Vitu vya Hali Yabisi chini ya HIPS.
Usahihi wa saa hiyo ulifikia asilimia takriban 95.
Mtafiti wa maabara akijaribu saa ya mkononi ya kupima hali ya afya kupitia jasho huko Hefei, Mkoa wa Anhui wa China, Juni 20, 2024. (Xinhua/Qu Yan)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma