Lugha Nyingine
Jumba la Makumbusho ya makaburi ya chini ya ardhi kwenye Njia ya kale ya Hariri lafunguliwa Xinjiang (6)
URUMQI – Katika sehemu ya mita takriban nane chini ya mtaa wenye maduka mengi wa Mji wa Kuqa, Mkoa unaojiendesha wa Xinjiang Uygur, Kaskazini-Magharibi mwa China, kuna makaburi ambayo yamefunikwa tuli chini ya ardhi kwa zaidi ya miaka 1,700. Hata hivyo, leo makaburi hayo, ambayo kihistoria yanaanzia kwenye Njia ya Kale ya Hariri, yamefukuliwa na kuoneshwa kwenye Jumba la Makumbusho la kipekee.
Jumba hilo la makumbusho la chini ya ardhi la Makaburi ya Kale ya Enzi za Wei na Jin (220-420) limefunguliwa rasmi siku ya Jumatatu katika Wilaya ya Kuqa, sehemu ambayo hapo awali ilikuwa ya Dola ya Kale ya Qiuci.
Dola ya Qiuci, ambayo ilianzishwa katika karne ya pili KK na ilidumu kwa zaidi ya miaka 1,000, ilikuwa mojawapo ya madola 36 katika “Maeneo ya Magharibi”. Maeneo hayo katika Enzi ya Han (206 BC-220 AD) yalikuwa maeneo ya magharibi ya Mpaka wa Yumen, yakiwa ni pamoja na Xinjiang ya sasa na sehemu za Asia ya Kati.
Jumba hilo la makumbusho lenye mita za mraba 5,000 lilijengwa kwa ajili ya kulinda vyumba 15 vya matofali vya makaburi vilivyogunduliwa sehemu hiyo Mwaka 2007 wakati wa ujenzi wa barabara ya chini ya ardhi ya Youyi. Hilo lilikuwa moja ya magunduzi makubwa kumi mapya katika utafiti wa mambo ya kale ya China mwaka huo.
Makaburi hayo yanafanana na makaburi ya mtindo wa Enzi ya Han yenye vyumba vya matofali yaliyogunduliwa katikati mwa China na kando ya Ukanda wa Hexi. Ukanda huo una umbali wa karibu kilomita 1,000 katika Mkoa wa Gansu, kaskazini-magharibi mwa China, na katika mkoa wa Gansu, kuna Maeneo Matano ya Mali ya Urithi wa Dunia ulioorodheshwa na UNESCO, na pia kuna mapango ya kale 53 ya mawe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma