超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Habari picha: Uchoraji wa picha ndani ya chupa huko Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 17, 2024
Habari picha: Uchoraji wa picha ndani ya chupa huko Kunming, Mkoa wa Yunnan wa China
Sun Hongyan akichora picha ndani ya chupa ndogo katika chuo cha Sanaa huko Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Julai 3, 2024. (Xinhua/Hu Chao)

Uchoraji wa picha ndani ya chupa ndogo ni aina ya sanaa ya jadi ya China. Hapo awali ilihusisha chupa ndogo za ugoro ambazo zilikuwa na picha zilizochorwa na Maandiko ya Kichina yaliyoandikwa ndani ya chupa.

Uchoraji huo wa picha unafanyika kwa kupenyeza brashi maalum kupitia mdomo wa chupa. Mchakato wa uchoraji, ambao hufanyika kwa kuijongesha brashi kabisa ndani ya chupa, ambapo mchoraji atatakiwa kuchora picha kwa usahihi kabisa.

Sun Hongyan, mchoraji mwenye umri wa miaka 49, amechora picha mbalimbali za mandhari za mazingira ya asili, mila na desturi za kikabila za Yunnan katika kazi zake za uchoraji picha ndani ya chupa ndogo, na hivyo amebuni uchoraji picha wa mtindo wa kipekee wa Yunnan wa sanaa hii.

Wakati wa kushikilia mbinu za jadi, wachoraji wamefanya ubunifu mpya, hivyo uchoraji picha ndani ya chupa unakaribishwa zaidi miongoni mwa vijana. "Tunainua uchoraji wa picha ndani ya chupa kwenye kiwango cha juu zaidi, tukichanganya ufundi huu wa kale na uzuri na sura mpya za zama tulizonazo," Sun amesema.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha