Lugha Nyingine
Kijiji kidogo cha Watu wa kabila la Wamiao chahimiza ustawishaji na maendeleo zaidi ya kijiji (10)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 19, 2024
Mwanakijiji Pan Meilan (wa kwanza, kulia) akimvalisha bintiye kwa ajili ya kushiriki kwenye shughuli za jadi katika Kijiji cha Wuying kwenye mpaka kati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini-Magharibi mwa China na Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Februari 12, 2024. (Xinhua/Huang Xiaobang) |
Kijiji cha Wuying katika eneo la mpaka kati ya Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wazhuang wa Guangxi, Kusini-Magharibi mwa China na Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, kikiwa na historia ya zaidi ya miaka 200, ni kijiji kidogo cha watu wa Kabila la Wamiao, ambacho kiko kwenye eneo la milima mirefu inayovuka mpaka kati ya mikoa ya Guangxi na Guizhou.
Hapo awali, milima na mazingira magumu yasiyoweza kupitika yaliwafanya wenyeji wa huko kuwa maskini sana. Katika miaka ya hivi karibuni, Kijiji cha Wuying kimefanya juhudi zaidi katika kuendeleza uchumi, elimu, utamaduni na mshikamano wa kabila, na kadhalika kuhimiza ustawishaji wa kijiji na kupata maendeleo zaidi.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma