Lugha Nyingine
China yarusha kwa mafanikio kundi jipya la satalaiti kwenda anga ya juu (4)
TAIYUAN - China imetuma kundi jipya la satalaiti kwenda anga ya juu siku ya Jumanne kutoka Kituo cha Kurusha Satalaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa nchi hiyo ambapo satalaiti hizo 18 ni kundi la kwanza la kizazi cha kwanza cha satalaiti za Spacesail ambazo zitawapa watumiaji wa kimataifa huduma za intaneti ya kasi ya kuchakata data kubwa kwa haraka, kasi kubwa na yenye ufanisi mkubwa, Kampuni ya Great Wall ya China ambayo ni mtoaji huduma hiyo imesema.
Satalaiti hizo zilirushwa majira ya saa 8:42 Mchana (Kwa saa za Beijing) zikiwa zimepakiwa ndani ya roketi iliyoboreshwa ya kubeba mizigo ya Long March-6 na kuingia kwa mafanikio kwenye obiti yake iliyopangwa awali.
Urushaji huo unamaanisha ni safari ya 530 kwenda anga ya juu kwa roketi za kubeba mizigo za Long March.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma