超碰caoporen国产公开,国产乱子伦精品免费视频,日韩美女一级黄片,丰满少妇棚拍无码视频

Jeshi la Sudan lahamisha waumini 6 wa kanisa katoliki wa Italia kutoka Khartoum (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 07, 2024
Jeshi la Sudan lahamisha waumini 6 wa kanisa katoliki wa Italia kutoka Khartoum
Waumini wa kanisa kutoka Italia waliohamishwa kutoka kusini mwa Khartoum wakiwa kwenye eneo la serikali katika Mji wa Omdurman, Sudan, Agosti 6, 2024. (Vikosi vya Wanajeshi vya Sudan/ Xinhua)

KHARTOUM - Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza siku ya Jumanne kuwahamisha waumini sita wa kanisa katoliki wa Italia na raia 20 wa Sudan Kusini ambao walikuwa wamekwama kusini mwa Khartoum tangu kuzuka kwa vita mwezi Aprili mwaka jana.

"SAF na Idara kuu ya Ujasusi (GIS) imehamisha watawa watano wa Jumuiya ya Wakatoliki wa Italia, kasisi kutoka Jumuiya ya Don Bosco ya Italia, na raia 20 wa Sudan Kusini kutoka kusini mwa Khartoum," Nabil Abdalla, msemaji wa SAF amesema katika taarifa.

Watu hao waliohamishwa walikuwa wamekwama kwa takriban mwaka mmoja na nusu katika eneo la Al-Shajara huko Dar Maryam, jengo la huduma mbalimbali lenye shule ya chekechea na ya msingi ikiwa ni sehemu ya mradi wa huduma ya elimu. SAF na GIS zimekuwa zikiwapa matibabu, chakula, na vifaa vya kuzalisha umeme kwa nishati ya jua.

Mwezi Desemba 2023, Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu lilijaribu kuhamisha kundi hilo, lakini operesheni haikufaulu kwa sababu wanamgambo wa Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) lililenga msafara wao, kwa mujibu wa taarifa ya SAF.

Taarifa hiyo inasema kuwa mamlaka ya Sudan ilipokea ombi rasmi kutoka kwa kanisa la Katoliki la Italia kuhamisha waumini wake kutoka kusini mwa Khartoum. Jeshi la Sudan limefanikiwa kuhamisha kundi hilo hadi Omdurman kabla ya kuwasafirisha hadi Port Sudan, mji mkuu wa Jimbo la Bahari Nyekundu mashariki mwa Sudan.

Eneo la Al-Shajara, ambalo linajumuisha kambi ya kimkakati ya askari wenye silaha, bado ni uwanja wa vita wa mapigano yanayoendelea kati ya SAF na RSF.

Sudan imekuwa ikishuhudia mgogoro mbaya kati ya SAF na RSF tangu Aprili 15, 2023, na kusababisha vifo vya watu 16,650. Watu takriban milioni 10.7 sasa ni wakimbizi wa ndani nchini Sudan, huku wengine takriban milioni 2.2 wakitafuta hifadhi katika nchi jirani, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizotolewa na Umoja wa Mataifa.?

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha